RAIS SAMIA AANDIKA HISTORIA MPYA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameweka historia mpya kwa kuwa Rais na Amiri Jeshi mwanamke wa kwanza toka Tanzania ilipopata Uhuru wake mwaka 1961 kuhutubia Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa.
Rais Samia aliyezaliwa Januari 27, 1960 (kwa mujibu wa mtandao wa wikipedia) aliingia madarakani mwaka huu baada ya Kifo cha aliyekuwa Rais wa awamu ya tano nchini Tanzania Hayati John Pombe Magufuli aliyefariki mwezi Machi 2021.
Rais Samia yuko nchini Marekani na amehutubia mkutano wa 76 wa
Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, katika Ukumbi wa Umoja wa Mataifa Jijini New
York,Marekani Septemba 23,2021. Rais huyo ameongozana na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Liberata Mulamula.
Post a Comment