WAVUVI 12 WAPOTEZA MAISHA BWAWA LA MTERA.
Wavuvi
12 wamepoteza maisha na wengine 15 kujeruhiwa katika kipindi cha mwezi
wa pili 2020 hadi mwezi wa nane 2021 kufuatia matukio ya kuvamiwa na Viboko wakiwa ndani ya Bwawa hilo katika shughuli za uvuvi.
Taarifa hiyo imetolewa ziara Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo
ya kukagua Jitihada za Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania TAWA
za kukabiliana na wanyama waharibifu na wakali amewataka wavuvi
kuzingatia njia sahihi za uvuvi salama ili kujilinda.
Moyo
alibainisha kuwa miongoni mwa sababu za matukio hayo yalioondosha uhai
ni pamoja na shughuli za Uvuvi kufanyika kwenye mazizi ya viboko,tabia
ya wavuvi kutumia zana duni za uvuvi,kupungua kwa samaki katika Bwawa
hilo na wavuvi kufanya shughuli ya uvuvi nyakati za usiku ambapo viboko
wanakuwa katika harakati za kutoka nje kutafuta chakula.
Moyo
aliyetembelea Bwawa la Mtera katika ziara ya kukagua jitihada za ziara
yake ya kukagua Jitihada za Mamlaka ya Usimamizi Wanyamapori Tanzania
TAWA za kukabiliana na wanyama waharibifu na wakali wakiwemo Viboko na
Tembo ameeleza kusikitishwa na matukio hayo huku akitaja miongoni mwa
sababu zinazochochea kuwapo kwa hatari dhidi ya wavuvi.
Moyo Amewaagiza maafisa Uvuvi, viongozi wa Serikali kwa ngazi zote
kusimamia na kuhamasisha njia bora za uvuvi katika Bwawa la Mtera ili
kuepuka migongano ya Wanyama pori wakali na waharibifu akisisitiza
kufuata miongozo na kanuni za uvuvi.
Post a Comment