MTANGAZAJI

MAFURIKO YATIKISA MAJIMBO MANNE MAREKANI

 

 
Takribani watu 46 wameshapoteza maisha  ndani ya saa 48  katika majimbo manne nchini Marekani kutokana na mafuriko yaliyosababishwa na Mvua kubwa iliyotokana na Dhoruba na Kimbuga Ida  kilichotokea usiku wa kuamkia Septemba 1 mwaka huu.
 
Watu waliopoteza maisha wanatoka katia majimbo ya  New York, New Jersey, Pennsylvania na Connecticut huku Kaya 150,000 zikikosa umeme.
 
Akizungumza kutoka Ikulu,Rais wa Marekani Joe Biden amesema " kimbunga kikali na janga la hali ya hewa viko hapa" na kuendelea kueleza kuwa "ni moja ya tatizo kubwa kwa wakati wetu" 
 
Kwenye mkutano na waandishi wa habari Alhamisi asubuhi Gavana wa New York Kathy C. Hochul amesema amepokea simu kutoka kwa Rais Baiden ambapo jimbo limefanya tathmini kutokana na kimbunga Ida ambacho kimesababisha madhara mapya ambapo jumatano mitaa na njia za treni kujaa maji na kuwa mito.
 
Katika jiji la New York huduma za usafiri wa treni inayopita chini ya ardhi imesitishwa .Viwanja vya ndege vilifunguliwa japo mamia ya Ndege zilisitishwa kutua ama kuondoka kwenye viwanja hivyo.
 
Alhamisi jioni Gavana wa New Jersey Philip D. Murphy ametangaza kuwa takribani watu 23 wamefariki katika jimbo hilo,miongoni mwao ni watu wanne ambao walikutwa wamefariki wakiwa ndani ya nyumba katika mji wa Elizabeth na wengine wawili huko Hillsborough baada ya kunasa kwenye magari yao.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.