WANAFUNZI WATAKIWA KUJENGA UJASIRI WA KUTOA TAARIFA ZA UKATILI
Naibu Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto nchini Tanzania Mwanaidi Ali Khamis ametoa agizo kwa wanafunzi hivi karibuni waliposhiriki ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Msingi Itunundu iliyopo Kijiji cha Itunundu Tarafa ya Pawaga Wilaya Iringa ikiwa ni sehemu ya kuamsha ari ya wananchi kujitolea kujiletea maendeleo.
Ripoti ya Jeshi la polisi nchini Tanzania inaonesha ongezeko la asilimia 25.95 la ukatili dhidi ya watoto. Katika mwaka 2020 visa 7388 viliripotiwa kote nchini tofauti na mwaka 2015 ambapo matukio 5,803 yaliripotiwa.
Ripoti ya Jeshi la Polisi inataja miongoni mwa ukatili dhidi ya watoto ulioripotiwa kwa kiwango kikubwa kuwa dhuluma za kingono ambapo katika mwaka wa 2020 kuliripotiwa visa 7263 ikiwa ni ongezeko la asilimia 26 ikilinganishwa na mwaka 2015 ambapo vilirekodiwa visa 5803, hii ikiwa ni sawa na visa 615 kwa mwezi jambo ambalo linatajwa kuwa linahatarisha mustakabali wa ustawi kwa watoto nchini humo.
Post a Comment