MTANGAZAJI

AJALI YA MOTO YASABABISHA KIFO CHA KIONGOZI WA KANISA LA WAADVENTISTA NA MKEWE

Huduma ya Ibada ya Faraja kwa wafiwa na kuona miili ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Konferensi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato ya Allegheny Mashariki (AEC), Henry J.Fordham III na Mkewe Sharon Elaine waliofariki kwa ajali ya Moto imepangwa kufanyika Agosti 8,2021 huko Baltimore, Maryland nchini Marekani.

 Usiku wa Julai 18 mwaka huu, Henry J. Fordham III na Mkewe Sharon Elaine Fordhan walifariki dunia kutokana na ajali ya moto iliyotokea nyumbani kwao Douglassville,Pennsylvania.

Kijana wao wa kiume Shawn Fordham ambaye alikuwa nao wakati moto unatokea nyumbani alipata majereha na kupelekwa hospitalini ambako alipatiwa matibabu kutokana na athari za moshi na hali yake ni nzuri kwa sasa .Bado chanzo cha moto huo hakijahamika ingawa uchunguzi bado unaendelea.

Kabla ya kifo chake Fordham alikuwa akihudumu katika nafasi ya Mwenyekiti wa AEC wadhifa ambao aliupata toka mwaka 2012.

 Baada ya kuhitimu shahada ya Thiolojia na Historia katika Chuo Kikuu cha Oakwood huko Huntsville, Alabama mwaka 1973 aliendelea na masomo kwa kujiunga na Chuo Kikuu cha Ohio ambako alihitimu shahada yake ya pili ya Thiolojia ya Kiyahudi. 

Fordham alitumia muda wa miaka 47 ya huduma akihudumu katika Konferensi ya Allegheny Mashariki kwa nafasi za Ualimu,Mchungaji,Ukurugenzi wa Idara na Kiongozi.

Kwa miaka miwili alifundisha Historia katika Shule ya Pine Forge ambapo alisoma miaka ya nyuma, Amewahi kuwa Mchungaji wa Makanisa ya Waadventista ya Sharon Temple huko Wilmington, Emmanuel-Brinklow Ashton na Berea Temple liloloko Baltimore. 

Kutoka Berea alichaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Huduma,Huduma Binafsi na Uhuru wa Dini wa AEC. Kisha baadaye akachaguliwa kuwa Katibu Mkuu wa Konferensi hiyo nafasi aliyoiongoza kwa miaka kadhaa kabla ya kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti ambapo pia alikuwa mmoja wa wajumbe wa Bodi ya Chuo Kikuu cha Oakwood,Chuo Kikuu cha Washington na taasisi mbalimbali za Kanisa la Waadventista wa Sabato.

Enzi za Uhai wake Fordham amewahi kushiriki kwenye mikutano mikubwa ya Injili nchini Afrika Kusini,Afrika Mashariki,Afrika Magharibi,Uingereza, Australia, Puerto Rico,Amerika ya Kusini na India.

Sharon Fordham alikuwa mtumishi wa ofisi za serikali ya Marekani zinazohusiana na masuala ya kijamii kwa miaka mingi katika jiji la Baltimore.

Fordham na mkewe ambao wote walikuwa na miaka 77 kila mmoja wakati wanafariki wamedumu katika ndoa yao kwa muda wa miaka 58 .




No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.