MTANGAZAJI

IDADI YA VIFO YAONGEZEKA UJERUMANI NA UBELGIJI

 

 

 Waokoaji wameendelea na kazi ya kurekebisha na kusaidia jamii kutokana na  uharibifu uliosababishwa na mafuriko huko Ulaya Magharibi huku idadi ya vifo ikiendelea kuongezeka na kufikia 160 na wakiwa bado wanatafakari muda watakaoutumia kusaidia jamii iliyoathirika na mafuriko ya jumatano katika eneo hilo.

Idadi ya watu waliopoteza maisha huko Magharibi mwa Ujerumani katika  jimbo la Rhineland-Palatinate,kitongozi cha Ahrweiler imeongezeka na kuwa 98,watu wengine 43 wamethibitishwa kufariki karibu na jimbo la Rhine-Westphalia Magharibi,huku Mamlaka inayohusika na majanga nchini Ubelgiji imeeleza kuwa idadi ya watu 27 wameripotiwa kufariki.

 Mara tu baada ya mafuriko kupiga Ujerumani na Ubelgiji  Jumatano na Alhamisi,Mamlaka nchini Ujerumani ilitoa idadi kubwa ya watu waliokuwa hawajulikani waliko jambo lililosababisha mkanganyiko,utoaji wa habari nyingi na ugumu wa mawasilino katika maeneo yaliyoathiriwa ambapo maeneo mengine yalikosa umeme na huduma za simu.

Hadi Jumamosi mamlaka zilikuwa bado na wasiwasi kuwa huenda idadi ya watu waliofariki kutokana na mafuriko hayo ikaongezeka jambo idadi inaendelea kupungua ingawa hawakuotoa idadi kamili.

Huko Ubelgiji watu 103 walielezwa kuwa hawajulikani walipo,japo kituo cha Majanga kilieleza kuwa kupotea kwa simu za raia  na zingine kutofanya kazi na watu kupelekwa hospitalini bila kuwa na utambulisho rasmi nayo imesababisha sintofahamu ya idadi kamili.

Mashariki mwa Ubelgiji reli na barabara bado hazipitiki kutokana na kuharibiwa na mafuriko.

Jumamosi hii Rais wa Kamisheni ya Ulaya Ursula von der Leyen na Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo wametembelea miji iliyoathiriwa na mafuriko hayo.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.