MTANGAZAJI

MAFURIKO YATIKISHA UJERUMANI NA UBELGIJI

 

 

Takribani watu  69 wamefariki Dunia  kutokana na mvua kubwa iliyosababisha mafuriko nchini Ubelgiji na Ujerumani.

 Watu 58 wameripotiwa kupoteza maisha nchini Ujerumani katika eneo ambalo lilipigwa na kimbunga na wengine 11 wakipoteza maisha nchini Ubelgiji.
Maofisa wa serikali wameeleza Alhamisi ya juma hili kuwa hawafahamu walipo watu  1,300.
Kimbunga kilisababisha kuharibika kwa miundo mbinu kikifuatiwa na mafuriko na kusabababisha majengo kuanguka na watu kujikuta wakiwa katika mapaa ya nyumba.
Kansela wa Ujerumani Angela Merkel akiwa katika ziara ya kikazi katika jiji la Washington Marekani  ameeleza kusikitishwa kwake na  watu waliopoteza maisha katika tukio hilo nchini mwake.
Madhara ya tukio hilo bado hajafahamika kwa undani,vyombo vya habari vimegundua kuwa wengi wa waliopoteza maisha waligundulika baada ya mafuriko na maji kupungua.
Timu za uokoaji zikiwa na helkopta zilijipanga kutoka Ufaransa siku ya jumatano kwa ajili ya kusaida uokoaji zikiungana na Italia na Austria ambazo zimetoa timu ya uokoaji.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.