MTANGAZAJI

FACEBOOK YAPANGA KUTOCHAPISHA MASUALA YA ASASI ZA KIRAIA NA SIASAMmiliki wa Mtandao wa Facebook  Mark Zuckerberg ametangaza jumatano ya juma hili kuwa Kampuni yake haitayakubalia makundi ya asasi za kiraia na siasa kwa watumiaji wa mtandao huo.

Mabadiliko hayo yanafuatia vurugu zilizotokea katika Mji Mkuu wa Marekani Januari 6,mwaka huu.

  Zuckerberg amefafanua kuwa kwa sasa Kampuni yake inatafuta hatua za kupunguza idadi ya maudhui ya siasa ambayo watumiaji wa Facebook wanayaona kwenye mapachiko yanayohusu habari na kusisitiza kuwa miongoni mwa mirejesho ambayo wanaipata kwa sasa ni kuwa watu hawapendi siasa na vurugu kutokea kupitia uzoefu wa huduma zao. 
 
Facebook ambayo pia inamiliki mtandao wa Kijamii wa Whatsapp na Instagram inaelezwa kuwa na watumiaji  bilioni  2.74  kwa mwezi duniani ambapo mwaka huu inatimiza miaka 17 toka ilipoanzishwa  huku ikishika nafasi ya pili nyuma ya   Tiktok kwa kupakuliwa na watu wengi Duniani kwa mwaka 2020.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.