MTANGAZAJI

CHUO CHA UHASIBU ARUSHA KUSOMESHA WACHEZAJI

Rais wa TFF Wales Karia (Kushoto )na Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof. Eliamani Sedoyeka Kulia Wakionesha Mkataba wa Ushirikiano Waliosaini Kuendeleza Mchezo wa Soka Baina ya Taasisi hizo  Januari 27,mwaka huu

 Mkuu wa Chuo cha Uhasibu Arusha Prof Eliamani Sedoyeka amesema Chuo hicho kwa kushirikiana na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kimepanga kutoa ufadhili wa masomo kwa vijana watakaofanya vizuri katika soka kwa mwaka wa masomo wa 2021/2022.

Pro Sadoyeka ametoa ahadi hiyo wakati wa  kusaini mkataba wa makubaliano ya ushirikiano na Shirikisho la Soka nchini (TFF) ili kuendelea kukuza michezo nchini Tanzania ambapo TFF watasaidia katika kuwapata vijana hao na chuo kitawapa ufadhili wa masomo kwa upande wa ada na malazi.

“Mwaka ujao wa masomo wa 2021/2022, tumepanga kutoa ufadhili wa masomo kwa vijana watakaofanya vizuri katika soka, na TFF watatusaidia katika kuwapata vijana hao, chuo kitawapa ufadhiri wa masomo kwa upande wa ada na malazi” alisema Prof. Sedoyeka.

 Akizunzungumza mara baada ya utiwaji wa saini makubaliano hayo Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Innocent Bashungwa amepongeza hatua hiyo ya Chuo cha Uhasibu Arusha kuunganisha taaluma na sekta ya michezo hatua inayosaidia kulea, kukuza na kuendeleza vipaji katika michezo mbalimbali.

 “Tutakitumia chuo hiki kama mfano kwa kufanikiwa kuunganisha mnyororo wa thamani kati ya taaluma na michezo, hatua hii ni mfano wa kuigwa na vyuo vingine nchini ili kiuandaa wanataaliuma na wanamichezo ambao wataleta tija kwa taifa kwa kujiongezea vipato vyao na pato la taifa” alisema waziri Bashungwa.

Rais wa Shirikisho la Soka nchini TFF Wales Karia amesema mkakati huo wa Chuo cha Uhasibu Arusha ni jawabu la kusimamia na kuendeleza wanamichezo ambao walikuwa wanapotea baada ya kumaliza kidato cha nne au cha Sita.

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.