MTANGAZAJI

GAZETI LA TAASISI YA HABARI YA WAADVENTISTA NCHINI TANZANIA LAANZA KUSAMBAZWA






Taasisi ya Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista wa Sabato Tanzania (TAMC)  imeanza kusambaza  Gazeti jipya liitwalo Sauti Kuu katika maeneo mbalimbali jijini Dar es salaam nchini Tanzania hii leo.

TAMC inayomilikiwa na Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini Tanzania ndiyo ambayo inasimamia Morning Star Radio na Kituo cha Televisheni cha Hope Channel Tanzania vilivyopo jijini Dar es salaam,Rock FM ya jijini Mbeya na Studio za Redio ya Waadventista Ulimwenguni (AWR) zilizoko Morogoro.

  Uzinduzi rasmi wa Gazeti hilo ambalo litakuwa likitoka mara moja kwa juma likiwa na habari mbalimbali za kijamii,kiroho,burudani na makala za Afya na Familia unatarajiwa kufanyika leo Mbweni jijini Dar es salaam zilipo ofisi za Unioni ya Kusini mwa Tanzania ya Kanisa la Waadventista wa Sabato nchini humo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.