MTANGAZAJI

WIMBO MPYA WA THE LIGHT BEARERS TOKA TANZANIA (+VIDEO)

Hii ni  video ya wimbo mpya wa waimbaji wa The Light Bearers toka nchini Tanzania ambayo ilichukuliwa mbashara na Versed Multimedia walipokuwa wakiimba kwenye Kanisa la Waadventista wa Wasabato Magomeni Mwembechai jijini Dar es salaam.

Baadhi ya wadau wanaowafuatilia waimbaji hao  wanaeleza kwenye mitandao ya kijamii kuwa wimbo huo uliopewa jina la Siku Moja  uko katika aina tofauti ya uimbaji wa nyimbo zao zilizotangulia toka toleo lao la kwanza la mwaka 2015.

 Santuri Mwonekano mpya ya The Light Bearers ambayo imetayarishwa na kutengenezwa na Mtayarishaji toka Uingereza Tegemea Champanda ambaye alikuja nchini Tanzania kuwarekodi waimbaji  hao hivi karibuni jijini Dar es salaam inasubiriwa kwa hamu kwa kuwa album hiyo itakuwa na nyimbo zilizotungwa na walimu toka Tanzania,Uganda na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC)

Akizungumza toka Uingereza,Tegemea Champanda amesema kuwa kwa sasa bado anaendelea na uhariri album hiyo ambayo audio yake imerekodiwa na JCB Studioz za jijini Dar es salaam.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.