MTANGAZAJI

MLEZI WA MWANAFUNZI MTANZANIA ALIYEFARIKI NCHINI MAREKANI AELEZA KUHUSU TUKIO HILO (+VIDEO)

Daudi Mayocha ambaye  alikuwa mlezi wa Allen Buberwa (22) aliyepoteza maisha baada ya kuzama katika Mto Buffalo ulioko Arkansas, Marekani ameeleza alivyopokea tukio hilo huku akitoa shukrani kwa upendo ulioonyeshwa na watanzania wakati wa msiba huu.

Mwili wa Allen aliyefariki jumatatu ya Mei 6 mwaka huu baada ya kuzama katika eneo la mto huo liitwalo  Pruitt Landing kilomita 169 toka Kaskazini Magharibi mwa jiji la Little Rock,Arkansas unatarajiwa kusafirishwa kwenda Tanzania jumanne wiki hii kwa Ndege ya Shirika la Ndege la Emirates na kufikishwa Dar es salaam jumatano kwa ajili ya taratibu za maziko.

Buberwa aliingia Marekani Disemba mwaka jana na akajiunga katika Chuo cha Arkasas  kilichopo karibu na Mji wa Harrison akiwa miongoni mwa wanafunzi wanaotoka mataifa mbalimbali nje ya nchi hiyo waliokuwa wakisoma taaluma ya utabibu. 

 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.