MTANGAZAJI

AFRIKA YA KUSINI NA KENYA WASAINI MKATABA WA KUFUNDISHA KISWAHILI SHULENI

 

Afrika ya Kusini itaanza kufundisha Lugha ya Kiswahili katika mfumo wake wa elimu baada ya kuingia makubaliano na Kenya.

Hatua hii inafuatia kikao kilichofanyika katika Mji Mkuu wa Kenya ambapo Katibu wa Baraza la Elimu nchini humo Prof George Magoha na Waziri wa Elimu ya  Msingi na Sekondari wa Afrika ya Kusini Angelina Matsie Motsie Motshekga kusaini mkataba wa makubaliano baina ya nchi hizo mbili.

 Akizungumza ofisini kwake Nairobi baada ya makubaliano hayo  Prof  Magoha alisisitiza kuwa  hiyo ni hatua ya maendeleo katika  kuimarisha ushirikiano baina  ya nchi hizo mbili.

Septemba mwaka jana Waziri Motshekga alitangaza kuwa Kiswahili kitaanza kufundishwa nchini Afrika ya Kusini ifikapo mwaka 2020.

Motshekga anatabainisha kuwa asilimi 40 ya wanafunzi nchini Afrika ya Kusini wanajifunza Kiswahili ama wanazungumza lugha hiyo.

Waziri huyo anaeleza mkataba huo utawezesha wanafunzi kuchagua Kiswahili kama ilivyo kwa lugha ya Kifaransa na Kireno.
Chanzo:CGTN

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.