MTANGAZAJI

VIJANA ZAIDI YA 1200 WA KIADVENTISTA JIMBONI TEXAS WAUNGANA NA KUTOA HUDUMA KWA JAMII Zaidi ya vijana 1,200 wadogo na wakubwa nchini Marekani katika jiji la nne kwa ukubwa walikutana kwa pamoja kwa ajili ya kutoa shuhuda ambavyo vilabu vyao vya watafuta njia na makundi ya vijana walivyosambaza upendo wa Kristo katika siku ya Kimataifa ya Matendo ya Huruma ya Vijana katika Kanisa la Waadventista wa Sabato Duniani (GYD) yenye lengo la kuwatia moyo vijana duniani kote "Kuwa Hubiri"katika jamii zao kama alivyofanya BWANA YESU.

Mkutano huo ulifanyika mchana ya Machi 16,2019 katika Kanisa la Waadventista wa Sabato la World Harvest Outreach mjini  Houston, Texas. Vijana mbalimbali toka makanisa ya Konferensi ya Texas na ile ya Kusini Magharibi walitoa taarifa  na visa mbalimbali vya namna walivyotoa huduma kwa jamii mapema siku hiyo.

Tyrose Douglas ambaye ni Mkurugenzi wa Idara ya Huduma za Vijana katika Konferensi ya Kusini Magharibi amesema ilikuwa ni jambo la kuvutia kuwaleta pamoja vijana toka Makanisa yanayotumia lugha ya kihispaniola na Kiingereza kwa ajil ya huduma kwa jamii.

Vijana hao walitoa taarifa ya namna walivyotoa huduma kwa vituo vya zimamoto,vituo vya Polisi,Hospitali na kuomba na wagonjwa,Polisi,wahudumu wa Afya na Madaktari .

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.