TAMASHA LA UIMBAJI WA KWAYA ZA KIADVENTISTA KUFANYIKA HOUSTON,TEXAS
Kwaya ya Kanisa la Waadventista wa Sabato la Umoja Central itasafiri umbali wa maili zipatazo 1,177 kuelekea kusini mwa Marekani katika jiji la Houston,Texas ambako kutakuwa na Tamasha la Uimbaji na mafundisho ya Kiroho katika Kanisa la Waadventista wa Sabato la Nations of Praise lililoko jijini humo kuanzia April 19 hadi 20 mwaka huu.
Akizungumza kwa njia ya simu toka Raleigh,North Carolina iliko kwaya hiyo inayojumuisha waimbaji toka Kenya na Tanzania, Mwalimu wa Kwaya ya Umoja James Owino amesema kwa sasa wako katika maandalizi ya kuhakikisha wanajiweka sawa kwa ajili ya Tamasha hilo ambalo pia litaihusisha kwaya ya Voices of East Africa ambao ndio wenyeji ikiwa na waimbaji wanaotoka katika nchi za Kenya,Tanzania na Jamaica.
Uongozi wa Kanisa la Nations of Praise umeeleza kuwa hii itakuwa ni nafasi ya pekee kwa mwaka wa 2019 kushuhudia uimbaji wenye vionjo vya kutoka Afrika hasa ukizigatia kuwa kwaya zote mbili zinaimba nyimbo kwa Lugha ya kiswahili.
Mwaka jana 2018 Kanisa hilo liliileta kwaya ya Ambassadors of Christ toka Rwanda ambayo ilitoa huduma ya umbaji kwa muda wa juma moja kanisani hapo na mwaka 2017 wakiwaleta Light Bearers toka Tanzania ambao walitoa huduma ya uimbaji kwa siku saba.
Post a Comment