MTANGAZAJI

SABA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI KUTOKANA NA TUKIO LA MAUAJI KATIKA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO

Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida Kamishina Msaidizi Sweetbert Njewike ametoa taarifa ya kuuawa kwa kupigwa risasi kwa Isaka Petro (28) kilichotokea kwenye Kanisa la Waadventista wa Sabato katika  kijiji cha Kazikazi,Manyoni mkoani Singida.

Taarifa ya kamanda Njewike imeeleza kuwa mauaji hayo yalitokea kanisani hapo Februari 2,2018 saa 8:20 mchana na jeshi la Polisi likiwashikilia watu saba kwa mahojiano kutokana na mauaji hayo.







Gazeti la Mwananchi toleo la Februari 5,2019 katika tovuti yake limendika kuhusu tukio hilo ambapo limewanukuu Waziri wa Ofisi ya Rais (Tamisemi) Suleimani Jafo,Mkuu wa Mkoa wa Singida Rehema Nchimbi na Mchungaji wa Kanisa la Waadventista wa Sabato anayesimamia kanisa ambako mauaji yalitokea Mch Manyigina Manyigina





No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.