CHAVITA YAIOMBA SERIKALI YA TANZANIA KUWAWEZESHA KWA KUWAPATIA MIKOPO YA FEDHA
Baadhi ya washiriki wa Semina ya Elimu ya Sera ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa makundi maalum wakifuatilia kwa makini mafunzo hayo yaliyoandaliwa na Wizara ya Fedha na Mipango , Jijini Mwanza. |
Mwenyekiti wa Chama cha watu wenye ulemavu wa kusikia mkoani
Mwanza (CHAVITA) Jones George, ameiomba Serikali kuweka mazingira wezeshi kwa
wenye ulemavu wa kusikia kupata mikopo ili waweze kujikwamua kiuchumi.
Ombi la Jones Goerge amelitoa kwenye wa mafunzo ya elimu ya Sera
ya Taifa ya Huduma Ndogo za Fedha kwa watu wenye ulemavu wa kusikia
kwa lengo la kuwajengea uwezo na kushirikishwa katika Huduma Jumuishi za Fedha yanayoendeshwa na Wizara ya Fedha na Mipango nchini Tanzania yanayofanyika mkoani Mwanza.
Katibu Mtendaji wa Katibu Mtendaji wa Taasisi ya Maendeleo ya watu wenye ulemavu wa kusikia Tanzania (TAMAVITA), Kelvin Nyema, ameipongeza Serikali kupitia Wizara ya Fedha
na Mipango kwa kuandaa mafuzo hayo ambapo ameeleza kuwa
tatizo kubwa linaoowakabili ni
mawasiliano ambayo yanasababisha wasishirikishwe katika shughuli mbalimbali za
maendeleo na za kijamii.
Alisema hali ya watu wenye ulemavu wa kusikia ni
ngumu, hawana elimu yoyote ya masuala ya fedha na hawajui waanzie wapi huku
akibainisha kuwa kuna wakati wanaogopa kukopa kwa dhana kuwa wakikopa
watafungwa.
Post a Comment