MTANGAZAJI

WAZIRI ATUMIA NUKUU ZA BIBLIA KUWAPA "SOMO" MAJAJI WAPYA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Dkt.
John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Makamu wa Rais
Mhe.Samia Suluhu Hassan, Jaji Mkuu Profesa Ibrahim Juma, Katibu Mkuu
Kiongozi Balozi Dkt. John Kijazi, Waziri wa Sheria Profesa Palamagamba
Kabudi,Waziri wa TAMISEMI Seleman Jaffo, Jaji Kiongozi Dkt. Eliezer
Fereshi pamoja na Majaji wapya 6 wa Mahakama ya Rufani Majaji wapya
15 wa Mahakama Kuu,wakuu wa wilaya na wakurugenzi

Waziri wa Katiba na Sheria nchini Tanzania Prof Kalamagamba John Kabudi ametumia nukuu za kitabu cha Zaburi sura ya 52 na Zaburi sura ya 33 katika Biblia kwenye  hotuba yake fupi akiwataka majaji majaji 6 wa Mahakama ya Rufani na Majaji 15 wa Mahakama Kuu Tanzania waliopishwa na Rais wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli Ikulu kuwa wajiepushe na vitendo vya rushwa na wahakikishe wanatunza viapo vyao vya kazi.

Kwenye tukio hilo lililofanyika januari 29 mwaka huu Prof Kabudi pia ameiomba serikali kusaidia mchakato wa kuwepo kwa mahakama zinazohamishika nchini Tanzania (Mobile Court ) ili huduma za makahama ziweze kuwafikia wananchi mahala walipo kwa urahisi na kwa wakati muafaka,Ambapo Rais wa Tanzania alitoa ahadi ya kutoa magari yatakayotumika kwa ajili ya mahakama hizo.

Uapishwaji huo uliambatana  na kula kiapo cha uadilifu wa viongozi wa Umma kwa wakuu wa wilaya wawili na wakurugenzi 10 wa Halmashauri nchini Tanzania

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.