MTANGAZAJI

LHRC YALITAKA JESHI LA POLISI TANZANIA KUFANYA UCHUNGUZI WA KINA WA MAUAJI YA YA WATOTO NJOMBE



Kufuatia ya mauaji ya watoto 10 mkoani Njombe nchini Tanzania ,Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu nchini humo (LHRC) kimelitaka Jeshi la Polisi nchini Tanzania kufanya uchunguzi wa kina na kuwachukulia hatua kali watakaobainika kujihusisha na matukio hayo.

Kupitia ujumbe wa twitter LHRC imeeleza kuwa inakemea vikali matukio hayo kwa kuwa yanakiuka haki ya kuishi na kimeamua kuendesha kampeni maalum ya kupiga vitendo hivyo kupitia hashtag ya #HakiYaKuishi.




 Taarifa toka Njombe zinaeleza kuwa  watoto 10 wenye umri kati ya miaka miwili hadi sita wamechinjwa na kukatwa koromeo,seheu za siri,masikio na ulimi mwezi januari. 

Mkuu wa Mkoa wa Njombe Christopher Ole Sendeka ameiagiza Polisi kupitia upya leseni za waganga wa jadi na kuwakamata wanaojihusisha na kutoa maelekezo yanayosababisha vifo vya watoto kwa imani za kishirikina.

Kwa mujibu wa mkuu wa wilaya ya Njombe, Ruth Msafiri, mtu mmoja amekamatwa kuhusika na baadhi ya mauaji hayo.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.