WANANCHI WANAOISHI NDANI YA HIFADHI YA MISITU YA VISIWA VYA KOME NA MAISOME WATAKIWA KULIPA TOZO
Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii, Costantine
Kanyasu amewataka wananchi wanaoishi na kufanya shughuli za uzalishaji
mali ndani ya Hifadhi ya misitu ya Visiwa vya Kome na Maisome
vilivyoko wilayani Sengerema mkoa wa Mwanza kulipa tozo za serikali bila
kulazimishwa.
Kauli
hiyo ameitoa wakati alipokuwa akizungumza na wakazi wanaoishi ndani ya
Hifadhi ya Msitu wa Shigala ulioko Kome Mchangani ambayo ni kambi ya
wavuvi wakati alipofanya ziara ya kutatua kero zinazowakabili wananchi
wa maeneo hayo.
Mbunge
wa Jimbo la Buchosa Dkt. Charles Tizeba amemueleza Naibu Waziri hiyo
kuwa kumekuwepo na changamoto ya ulipaji tozo kubwa hata kama mtu ana
eneo dogo na ndipo wananchi walilazimika kugoma kulipa tozo hiyo kwa
lengo la kupata msaada zaidi.
Mtu anayemiliki hekari moja anatakiwa kulipa Tsh.425,000 kwa
mwaka lakini hata mtu anayemikili eneo dogo la mita 20 naye anatakiwa
kulipa kama wa hekari moja kitendo kilichowafanya wananchi hao
kushindwa kulipa na kusubili maelekezo ya wizara husika.
Mmoja
wa wananchi wanaoishi ndani ya Hifadhi hiyo,Juma Ramadhani amemwomba
Naibu Waziri kuangalia upya sheria hiyo ili wananchi wapate nafuu ya
kulipa na serikali iweze kupata mapato yake.
Kanyasu
amewahakikishia wananchi hao kuwa suala hilo atalipatia majibu kwa
haraka lakini amewataka watu wanaomiliki hekari moja kulipa tozo hizo
kwa wakati na wale wenye maeneo madogo madogo wajiunge katika vikundi
ili waweze kuilipa pesa hiyo
Post a Comment