RAIS RUTO AKABIDHI BARUA YA KUPANDISHA HADHI CHUO KIKUU CHA KAMAGAMBO
Rais wa Kenya, William Ruto, Septemba 15 mwaka huu, alikikabidhi Chuo cha Ualimu cha Kamagambo cha kanisa la Waadventista wa Sabato Barua ya Mamlaka ya Muda , hatua inayokipandisha rasmi kuwa Chuo Kikuu cha Kamagambo na kuwa miongoni mwa vyuo vikuu vya binafsi nchini humo.
Utoaji wa kibali hicho alichokikabidhi kwa Makamu Mkuu wa Chuo hicho Rei Towet Kesis mbele ya viongozi wandamizi wa Unioni Konferensi ya Kenya Magharibi ya Kanisa la Waadventista wa Sabato, watendakazi wengine wa chuo hicho na maafisa wa serikali, wakati wa ziara ya Rais Ruto katika eneo la Nyanza, ambapo alifanya mikutano na wadau mbalimbali katika jengo maalum la serikali la Kisumu.
Kupandishwa hadhi huku kunaiwezesha taasisi hiyo kuanzisha miundo ya uongozi wa chuo kikuu na, baada ya idhini ya Tume ya Vyuo Vikuu Kenya (CUE), kitaanza kudahili wanafunzi kwa ajili ya kutoa elimu za shahada mbalimbali.
Kamagambo ina historia ndefu katika taasisi za elimu za Waadventista nchini Kenya. Kazi ya elimu ya Waadventista katika eneo hilo ilianza mwaka 1912, na mafunzo rasmi ya ualimu yakaanza mwaka 1928. Chuo kikuu hicho kitaanza kwa kutoa elimu katika shahada tatu ambazo ni Shahada ya Elimu, Shahada ya Thiolojia na Ujasiriamali, Shahada ya Utawala wa Biashara na Ujasiriamali.

.png)
Post a Comment