MTANGAZAJI

MATUKIO YA ASKARI POLISI KUJIUA BADO NI TATIZO KATIKA JAMII


Takwimu za Polisi kujiua nchini Marekani ambazo zimetangazwa na CNN Januari 7,2019

Katika kipindi cha wiki moja (Julai 9 -13, 2018) matukio matatu ya askari polisi kujiua nchini Tanzania yaliripotiwa. Kiujumla Matukio ya watu kujiua yameendele kuwa moja ya mambo 10 yanayosababisha  ukiukwaji wa Haki ya Kuishi Duniani. 

Sababu kuu ya askari hao kujiua inatajwa kuwa Msongo wa Mawazo (psychological stress) unaosababishwa na watu kushindwa kukabiliana na changamoto mbalimbali za kijamii kama mahusiano/ndoa, pamoja na changamoto za kiuchumi ikiwemo ugumu wa maisha. Matukio haya kwa jeshi la polisi yamekuwa ya kujirudia mara kwa mara.


Kwa mujibu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) takribani watu laki 8 hadi milioni  1 hujiua kila mwaka kwasababu mbalimbali.


Kwa mujibu wa Sheria ya Kanuni ya Adhabu Sura ya 16, Kifungu cha 216 na 217: Kushawishi mtu Kujiua au Kujaribu Kujiua ni Kosa la Jinai. Kifungu cha 216 kinafafanua:

Mtu yeyote ambaye;

(a) anasababisha mtu mwingine ajiuwe; au (b) anamshauri mtu mwingine ajiuwe na akamshawishi kufanya hivyo; au (c) anamsaidia mtu mwingine ajiuwe, atakuwa anatenda kosa na atahukumiwa kifungo cha maisha.

Kujaribu kujiua, kifungu cha 217 kinafafanua: Mtu yeyote anayejaribu kujiua ana hatia ya kosa.

Takwimu zilizotangazwa na CNN Januari 7 mwaka huu zilieleza kuwa nchini Marekani kwa mwaka 2016 askari Polis 140 walijiua,ambapo kwa mwaka 2017 wajiua askari 159 na kwa mwaka 2018 askari waliopoteza maisha kwa kujiua walikuwa 160.

Wito kwa Jeshi la Polisi hasa nchini Tanzania ni kuboresha mazingira ya kazi ya maafisa wa jeshi hilo ili kuwaepushia msongo wa mawazo unaoweza kutokana na ugumu wa maisha na mazingira ya kazi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.