MTANGAZAJI

SERIKALI MKOA WA RUKWA YALIOMBA KANISA LA WAADVENTISTA KUONGEZA JITIHADA ZA KUTOA HUDUMA ZA KIJAMII NA KIROHO

Image may contain: one or more people, crowd and table
Waumini wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato waliohudhuria uzinduzi wa jimbo dogo la Majaribio la Lake Tanzania (LTF)
Serikali ya mkoa wa Rukwa imeliomba Kanisa la Waadventista wa Sabato kuongeza jitihada za kutoa huduma za kijamii na kiroho katika mkoa huo ili kusaidia maendeleo  katika nyanja za elimu na afya na kufundisha maadili mema katika mkoa huo.

Akizungumza kwa niaba ya mkuu wa Mkoa katika uzinduzi wa jimbo dogo la Majaribio la  Lake Tanganyika  (LTF) Katibu tawala wa mkoa wa Rukwa David Kilonzo amesema Serikali ina matarajio makubwa ya uboreshwaji wa huduma za kijamii baada ya jimbo hilo dogo la majaribio  kuzinduliwa katika halmashauri ya Sumbawanga. 
Kilonzo alieleza kuwa takwimu za miezi 3 iliyopita zinaonyesha jumla ya wanafunzi 72 wamepata ujauzito na kupoteza nafasi ya masomo mkoani humo  dalili ambayo ni kuporomoka kwa maadili.

Uzinduzi wa LTF itakayohusisha eneo la mikoa ya Rukwa,Songwe na Katavi uliongozwa na  Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista wa Sabato jimbo la Kusini mwa Tanzania Mch. Mark Malekana na makao yake makuu yatakuwa katika  halmashauri ya Sumbawanga mkoani Rukwa.

Katika uzinduzi huo,Mch. Malekana amewataka waumini wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika  jimbo hilo kufanya kazi kwa bidii ili kukuza uchumi binafsi na taifa kwa ujumla na kujiepusha na uvivu kwa kutumia muda mwingi katika kucheza michezo ya kubahatisha na kuongeza kuwa ni marufuku kwa muumini wa Kanisa la Waadventista wa Sabato  kucheza michezo ya bahati nasibu na badala yake wafanye kazi.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.