MTANGAZAJI

NDEGE YA PILI YA AIRBUS A220-300 ILIVYOPOKELEWA KATIKA UWANJA WA NDEGE WA JNIA JIJINI DAR ES SALAAM,TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na viongozi mbalimbali akikata utepe kuashiria kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 iliyowasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Januari 11, 2019

Maafisa waliokwenda Canada kuipokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 wakilakiwa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam l
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano na Uchukuzi Mhandisi Isaack Kamwelwe wakipewa maelezo na  Rubani Patrick kuhusu ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 walipoipokea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akipungia wananchi baada ya kupokea ndege ya pili ya AIRBUS A220-300 Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam Januari 11, 2019

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa na mkewe Mama Mary Majaliwa wakiwa na viongozi wengine mbalimbali wakishuka kutoka katika ndege ya AIRBUS A220-300 ilipowasili (Picha zote na Ikulu)

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.