MTANGAZAJI

AMBASSADORS OF CHRIST TOKA RWANDA WAWEKA HISTORIA HOUSTON,MAREKANI


       Moja wa nyimbo walizoimba Ambassadors of Christ


Watu waliohudhuria


Agosti 13,2018 imewekwa katika kumbukumbu kwa mara ya kwanza na Kanisa la Waadventista Wa Sabato la Nations of Praise lenye waumini 85 kwa mwaka huu kwa kufanya Tamasha la Uimbaji la Ufunguzi wa Mkutano wa Injili unaofanyika hapa Ashford katika jiji la Houston .

Tamasha hilo lililodumu kwa muda wa saa tatu ambapo  lilihudhuriwa na raia wengi toka nchi za Afrika Mashariki na Kati liliwashuhudia  waimbaji wa Ambassadors of Christ toka Kigali Rwanda,Emanuel,Violet Mark,Voices of East Africa,Houston International na Pearl Salene toka Afrika Kusini

Ikiwa ni juma lao la pili kuwepo hapa Marekani Ambassadors of Christ  waliimba nyimbo kwa muda usiopungua dakika tisini wakiwa wamegawanya nyimbo hizo katika ushuhuda  wa sehemu tatu kwa namna ambavyo safari yao ya uimbaji ilivyoanza mwaka 1995 mpaka sasa huku wakigusia utume wao kupitia uimbaji barani afrika na sasa nchini Marekani huku wakisimulia ajali ya gari iliyowapata nchini Tanzania na  kuwapoteza waimbaji wao watatu.

Hii itakuwa ni ziara ya kwanza kwa Waimbaji wa Ambassadors kuwepo nchini Marekani toka waanze kuimba.

Katika tamasha hili ambalo pia lilishuhudiwa na Mwinjilisti wa Kimataifa Dr Heri Muhando na mkewe ambao ndio wanenaji kwenye mkutano ulioanza leo Ambassadors of Christ waliimba nyimbo zao kwa lugha ya Kiswahili,Kilingala,Kiganda na Kinyarwanda huku tamasha hilo lililorushwa mbashara  likishuhudiwa na maelfu ya watu toka sehemu mbalimbali duniani  kupitia mtandao wa kijamii wa Facebook katika ukurasa maalum wa Kanisa la Nations of Praise ambao utakuwa ukitumika kurusha mkutano wa Dr Heri Muhando na Ambassadors of Christ kuanzia saa 12 jioni kwa saa za Houston,Marekani kwa juma zima toka kanisani hapo huku kukisubiriwa tamasha lingine la uimbaji siku ya ijumaa

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.