WADAU WAWASUBIRI KWA HAMU AMBASSADORS OF CHRIST NA DKT HERI MUHANDO JIJINI HOUSTON
Juma hili likiwa linaelekea kumalizika huku siku zikihesabika moja baada ya nyingine,hapa Houston kwa wale wapenda nyimbo za Injili wanasubiri kwa hamu kuwaona Ambassadors of Christ na Dkt Heri Muhando wakiwa hapa juma lijalo.
Kwa sasa Waimbaji hao toka Rwanda na Mwinjilisti Muhando wanaendelea na mkutano wa kwanza wa Injili unaofanyika Dallas hapa hapa Texas.
Katika mazungumzo na baadhi ya watu kutoka Afrika Mashariki na Kati walioko katika majimbo mengine mbali na hapa wameshaanza kufanya taratibu za kufika Houston kuwashuhudia waimbaji hao ambao wako ziara ya kwanza hapa Marekani pamoja na Dkt Heri Muhando toka Dar es salaam,Tanzania.
Dkt Heri Muhando alifanya mkutano mwingine wa Injili mwaka jana huko Minnesota ambapo walibatizwa watu wapatao 80.
Sikiliza Makala hii ambayo imefanywa hapa Houston,Texas nchini Marekani.
Post a Comment