WAADVENTISTA WA SABATO JIJINI MWANZA WANAVYOJIANDAA NA MKUTANO WA UFUNUO WA MATUMAINI
Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Jimbo Kuu la Kaskazini mwa Tanzania akihutubia waumini wa Kanisa hilo kwenye uwanja wa CCM,Kirumba Mwanza |
Kanisa la
Waadventista Wa Sabato toka mitaa 13 ya
jiji la Mwanza yenye makanisa mahalia 82 ambayo yanawaumini wapatao 33,308
walikusanyika kwenye uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza April 14 mwaka huu
katika Sabato maalum ya maandalizi ya mkutano wa Ufunuo wa Matumaini
utakaoendeshwa na Mwinjilisti wa Kimataifa Mark Finley toka nchini Marekani Mei
12 hadi June 2 mwaka huu uwanjani hapo.
Siku hii maalum ambayo pia ilihudhuriwa na kwaya zipatazo 54,
viongozi wa jimbo dogo la Nyanza Kusini lenye mikoa ya
Mwanza,Simiyu,Geita na Shinyanga hali kadhalika Viongozi wa Jimbo Kuu la Kusini
mwa Tanzania na Jimbo Kuu la Kaskazini katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato
wakiongozwa na Mwenyekiti wake Dr Gordwin Ole Lekundayo ambaye alitoa hotuba
maalum ya ibada iliyosisitiza kuhusu umuhimu wa Habari Njema.
Alisema watu hupenda kusikia habari njema, mama kajifungua mtoto, mtoto amefaulu
mitahani, nimepata mchumba, nimepanda cheo na mengine mengi husikia na
kuyaona. Katika ulimwengu huu wenye kuhuzunisha Je, habari njema
zinaweza kupatikana?,Hivyo mkutano wa Ufunuo wa Matumaini utaleta habari njema kwa jiji la Mwanza na Tanzania kwa ujumla.
-->
Post a Comment