WAKUU WA TEKNOHAMA WAKUTANA KENYA
Watunga sera na sheria mbali mbali wamekua wakifanya maamuzi ya TEKNOHAMA bila kushirikisha wadau wa TEKNOHAMA – Hii imekua moja ya changamoto inayo leta mkinzano wa utendaji wenye manufaa kwa wana TEKNOHAMA maeneo mengi barani Afrika.
Mjadala
ulioangazia umuhimu wa udhibiti na uangalizi wa watendaji katika sekta ya
TEKNOHAMA umeonekana kua mzuri ila umegubikwa na changamoto kadhaa kutokana na ushirikishwaji
mdogo wa wadau ili kuweza kuleta mabadiliko kwenye sekta husika.
Mjadala
huu umejadiliwa kufuatia kuwepo kwa sera mpya nchini Kenya itakayo rasimisha
Wana TEKNOHAMA na kuwataka watambulike kabla ya kuweza kuhudumu maeneo mbali
mbali. Hili litafanana na tulicho nacho nchini Tanzania kwa wanasheria pamoja
na wataalam wa maeneo mengine kadhaa.
Kinachotegemewa
katika urasimishaji wa sekta ya TEKNOHAMA na kumfanya mwana TEKNOHAMA
atambulike na kuhudumia katika sekta ya TEKNOHAMA ni pamoja na kupitia
hatua kuu tatu ambazo ni, Kusomea – Usaili – Kupatiwa leseni ya kutoa huduma
katika sekta husika.
Changamoto
iliyo onekana ni pamoja na uwezekano wa kuua vipaji vya wabunifu wa TEKNOHAMA
ambao wamekua wakija na ubunifu wenye manufaa pasi na kua na ujuzi rasmi katika
sekta husika.
Tumeshudia
kuwepo kwa vijana walio somea fani nyingine tofauti na TEKNOHAMA ila baadae
kuja na Mifumo mizuri ya Kitehama iliyoweza kutatua changamoto mbali mbali
katika maeneo yetu tofauti na wengine waliosomea fani husika na kushindwa kuwa
wabunifu wa kuleta mabadiliko katika jamii zetu.
Kuna
baadhi ya Mifumo tuko nayo maeneo mengi ambayo wabunifu wake hawakua na elimu
ramsi katika sekta ya TEKNOHAMA. Aidha, Swali kuu matumizi ya TEKNOHAMA ya
mekua kuna ulazima mhusika kua na elimu rasmi? Ilhali kila sekta inategemea
TEKNOHAMA na kuna uwezekano kila mwenye ujuzi wa fani yoyote akawa na uwezo wa
kufanya vizuri kwenye mifumo ya TEKNOHAMA.
GDPR
(General Data Protection Regulations) Nchi za umoja wa ulaya wana mategemeo ya
kuanza rasmi matumizi ya GDPR mwishoni mwa mwezi wa tano mwaka huu wa 2018 –
Lengo kuu ni kulinda faragha za raia wake.
Hatua
hii inaweza kuathiri maeneo mengi duniani Afrika ikiwemo kwani tumeendelea
kufanya biashara na kuhudumia mataifa ya umoja wa ulaya ambapo inahusisha
taarifa za wana jumuia ya ulaya kupatikana kwetu.
Mjadala
mzito wa nini tutegemee pale umoja wa Ulaya watakapo anza rasmi matumizi ya
GDPR katika taasisi zetu hususan za kifedha. Namna bora ya kuweza kulinda
(faragha) za watumiaji mifumo ya kitehama katika taasisi zetu ili kuondokana na
tunachoweza kukabiliana nacho baada ya kuanza rasmi matumizi ya GDPR barani
ulaya.
CSIRT
(Computer Security Incidence Response Team) – Tumekua na changamoto ya uwepo wa
vitengo mahususi vya kukabiliana na matukio ya kihalifu mtandao katika taasisi
na kampuni mbali mbali. Hili linatokana na uelewa mdogo juu ya umuhimu wa
vitengo hivi mahsusi vyenye jukumu la kukabiliana na uhalifu mtandao.
Umuhimu
wa CSIRT, namna ya kuanzisha na majukumu yake katika kila kampuni na taasisi ni
mjadala nilio uongoza kuhakiki kila mmoja anafahamu hili.
Matukio
ya kihalifu mtandao katika mataifa yetu yanayopelekea upotevu wa Fedha, upotevu
wa taarifa, udukuzi wa mifumo na kadhalika yamekua yakijitokeza mara kwa mara
yanayo acha athari kubwa kwa taasisi za serikali na binafsi maeneo mengi
duniani.
Ni
wajibu wa kila taasisi na kampuni kujua ina jukumu la kujilinda dhidi ya
uhalifu mtandao na namna pekee ya kufikia hapo ni pamoja na kua na kitengo
wahususi chenye jukumu la ulinzi mtandao pekee ambapo kitengo husika kitaweza
kuhakiki usalama mtandao unakuwepo.
Aidha,
kumekua na mijadala mingine mingi sana ambayo yote ilikua na lengo la kuhakiki
tuna tambua namna sahihi ya kukabiliana na changamoto nyingi zinazotokana na
uwepo matumizi makubwa ya mifumo ya TEKNOHAMA yanayo rahisisha utendaji kazi
katika taasisi na kampuni mbali mbali.
YUSUPH
KILEO
Post a Comment