WAZIRI MHAGAMA AZINDUA HUDUMA MPYA YA WCF YA WAAJIRI KUJISAJILI KWENYE MTANDAO WA INTERNET
Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, akielezea jinsi huduma hiyo iyakavyofanya kazi. |
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, (Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama, amezindua huduma mpya itakayowawezesha waajiri kujisajili na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), kwa kutumia mtandao wa Internet.
Mhe. Mhagama amezindua huduma hiyo leo Novemba 29, 2017, wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Mwaka wa Wadau wa Mfuko wa Fidia Kwa Wafanyakazi, (WCF), kwenye ukumbi wa Simba wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa, AICC, Arusha.
“Huduma hii itawawezesha waajiri kujisajili na Mfuko kupitia mtandao wa internet na hawalazimiki kujaza fomu na kuja ofisini kwetu au kwa maafuisa kazi” Mkuu wa kitengo cha Tehama cha WCF, Bw. Stephen Goyayi, alisema wakati akitambulisha huduma hiyo kwa Mhe. Waziri.
Katika hatua nyingine, Benki ya NMB Bank plc imenyakua tuzo baada ya kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi.
Kampuni zingine zilizonyakua tuzo kundi la waajiri ni Steel Master Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji nyaraka za madai ya fidia kwa wafanyakazi na kampuni nyingine ni KPMG Advisory Ltd kwa kuwa mwajiri bora katika uwasilishaji michango miongoni mwa kundi la waajiri wenye wafanyakazi wengi.
WCF iliwatunukia tuzo wadau wa Mfuko huo ambapo Waziri Jenista kwa niaba ya Serikali alipokea tuzo hiyo, kwa kutambua mchango wa Serikali katika kuanzisha na kufanikisha utendaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi.
Wadau wengine ni Shirika la Vyama vya Wafanyakazi, (ATE), Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi, (TUCTA), Mamlaka ya Usimamizi wa Hifadhi ya Jamii, (SSRA), kwa kutambua ushiriki wake katika uanzishwaji wa Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF)
Waziri Mhagama (watatu kushoto) na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Waziri Mkuu, Bw. Eric Shitindi, (wakwanza kushoro), wakipokea hundi yenye thamani ya shilingi milioini 33.8 kutoka kwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba, (wapili kushoto). Fedhab hizo ni kwa ajili ya kusaidia ununuzi wa komputa nundu (perkins Braille Machines) kwa ajili ya wanafunzi wenye ulemavu wa kuona katika shule za umma.
Baadhi ya wajumbe wa Bodi ya Wadhamini ya WCF,. Wakwanza kushoto ni katibu wa Waziri Jenista Mhagama.
Mheshimiwa Waziri Jenista Mhagama, akimkabidhi tuzo Bw. Richard L.Makungwa kutoka NMB Bank Plc tuzo ya mwajiri mwajiri bora katika uwasilishaji michngo miongoni mwa waajiri wenye wafanyakazi wengi. Kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mhe. Mrisho Gambo, na kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya WCF, Bw. Emmanuel Humba.
Mheshimiwa Waziri akimkabidhi tuzo Kaimu Mwenyekiti wa ATE, Bi. Janet Reuben Lekashingo tuzo ya ushiriki kama Mdau wa WCF. Anayeshuhudia ni Bw. Humba.
Mheshimiwa Waziri akimkabidhoi tuzo Kaimu Mwenyekiti wa ATE, Bw.Tumaini Peter Nyamhokya, Katibu Mkuu wa TUCTA, tuzo ya ushiriki kama mdau wa WCF. Anayeshuhudia ni Bw. Humba.
Mheshimiwa Mhagama akimkabidhi tuzo, Bw. Hiroshi Yamobana kutoka ILO kwa ushiriki na kama mdau
Waziri Jensita akipokea zawadi ya saa kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba
Mmoja wa watu wanaofaidika na Mafao ya WCF,
Post a Comment