MTANGAZAJI

EUNICE IRAKIZA BINTI MWENYE HISTORIA NDEFU NA TANZANIA,KUFUNGA NDOA NA MWIMBAJI WA AMBASSADORS OF CHRIST HII LEO





Utambulisho rasmi wa wanandoa watarajiwa kabla ya kufunga ndoa kwa mujibu wa taratibu za Rwanda

Eunice Irakiza  ambaye amedumu katika uchumba wa  miaka minne na Nelson Manzi mwimbaji wa Ambassadors of Christ wakitarajia kufunga ndoa hii leo,Binti huyu  alizaliwa na kukulia Kigoma nchini Tanzania wakati  wazazi wake na Babu yake Eunice alifia Kigoma ambapo wakati wa uhai wake alikuwa  Mchungaji mkoani humo.

Na wazazi wa Eunice walioana Kigoma na walikuwa wakifanya kazi katika Hospitali ya Heri ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tanzania na baadaye waliondoka kwenda Rwanda wakati huo ambapo  Eunice akiwa binti mdogo.

 Inaelezwa na mtu aliyewahi kufanyakazi pamoja na familia ya Eunice huko Kigoma  kuwa kuelekea mwaka  2000,Baba yake Eunice alikuwa Daktari katika zahanati iliyoko Kigoma mjini eneo la Mwanga ilipokuwa  ofisi ya kwanza kabisa ya Jimbo la Magharibi mwa Tanzania Kanisa la Waadventista Wa Sabato (WTC ) wakati huo ikiitwa Field ya Magharibi mwa Tanzania (WTF).Enzi hizo zahanati hiyo ilikuwa inamilikiwa Na WTC ila kwa sasa inamilikiwa na Hospitali ya Waadventista ya  Heri iliyoko Kigoma. 

Mama yake Eunice alikuwa ni Muuguzi hapohapo Kigoma Mjini. Pia Baba yake Eunice alishika nafasi za uzee wa kanisa la Waadventista Wa Sabato Kigoma. Kaka yake Eunice aitwaye Gadi Bakinahe ni mwimbaji wa waimbaji wengine wa Rwanda waitwao  Friends of Jesus na alianza kuimba akiwa mdogo sana akiwa  Kigoma,Tanzania.

 Baba yake Eunice (Mzee Waswa na Mkewe) walikuwa watumishi wa Heri Hospital kabla ya kuoana na Baadaye wakaoana hapohapo Heri Hospital. Baba yake Eunice akiwa Heri Hospital aliwahi kuwa mwimbaji Wa Kwaya ya Heri ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato  wakati huo akisoma Uuguzi (Nursing) na akiimba sauti ya nne na mama yake  Eunice alikuwa mwimbaji.

Ndoa ya Eunice na Nelson Manzi ambaye ni mwimbaji mahiri wa Ambassadors of Christ kwaya ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Rwanda akiimba pia na dada yake na mdogo wake wa kiume inataraji kufungwa leo saa 8: 00 mchana katika kanisa la Kiingereza la Kigali (Kigali English SDA Church) na kufuatiwa na tafrija itayofanyika saa moja katika ukumbi wa Green Hills Academy kuanzia saa 1:00 jioni kwa saa za Rwanda.



No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.