MTANGAZAJI

TAUS WAIDHINISHA MILIONI 60 KUFADHILI MIRADI MBAMBALI NCHINI TANZANIA MWAKA 2017/2018


Mkurugenzi wa Miradi wa TAUS Mch Caleb Migombo akiwa na Mmiliki wa Mtandao huu Mtangazaji Maduhu nchini Marekani wakati wa Kongamano la TAUS 2017

Kamati ya UtendajI ya Umoja wa Waadventista Watanzania nchini Marekani (TAUS)  imeidhinisha matumizi ya kiasi cha dola za kimarekani 26,800 sawa na shilingi milioni 60 za kitanzania kwa ajili ya kufadhili miradi mbalimbali ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato nchini Tanzania kwa kipindi cha mwaka 2017/2018.

Taarifa iliyotolewa hivi karibuni  na Mkurugenzi wa Miradi wa TAUS Mchungaji Caleb Migombo inaonesha kuwa miradi itakayonufaika na mkakati huo ni kuwasomesha wachungaji,kufanya mikutano ya injili,Ujenzi wa Makanisa,Ununuzi wa Vifaa vya Morning Star Radio na Upelekaji wa Injili katika maeneo mapya.

Taarifa hiyo imefafanua kuwa kati ya fedha hizo dola 5,000 zitakwenda kusaidia masuala ya Uinjilisti Nanyamba,Tandahimba mkoani Mtwara  katika jimbo la Kusini Mashariki mwa Tanzania (SEC) na Nchemba,Dodoma huku kiasi kama hicho pia kikipangwa kwa ajili ya ujenzi wa makanisa huko Tandahimba na Namtumbo mkoani Ruvuma.

Miradi mingine iliyopangwa na TAUS na kuanza kutekeleza hivi karibuni  ni matumizi ya dola 2,500 kwa ajili ya Ununuzi wa vifaa vya  Morning Star Radio,Dola 3,600 Kuwasomesha wanafunzi wa Uchungaji  4 kati ya 14 wanaonufaika na ufadhili huo walioko katika Chuo Kikuu cha Arusha na Bugema nchini Uganda pamoja na Ununuzi wa vipaza sauti vya Kanisa la Waadventista Wa Sabato Nchemba Dodoma vyenye thamani ya dola 2,500.

TAUS ilianzishwa mwaka 1999 huko Massachusetts Marekani na wanachama 25 kwa lengo la kuwaunganisha Waadventista Watanzania walioko nchini humo ambapo kwa sasa inawachama wapatao 300.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.