MTANGAZAJI

TANGA:UHARIBIFU WA VYANZO VYA MAJI VYAIGIZA HASARA TANGA UWASA YA MILIONI 13 KWA SIKU.



 Muonekano wa Maji kwenye chanzo cha Maji cha Mto Zigi

Mamlaka  ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga (Tanga
Uwasa)inapoteza kiasi cha shilingi milioni 13 kila siku kutokana na kuongezeka kwa za shughuli za kibinaadamu zinazofanywa katika vyanzo vya maji vilivyopo katika Mto zigi na Muzii Wilayani Muheza.

 
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea kwenye vyanzo vya maji,Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji na Usafi wa Mazingira Jijini Tanga(Tanga Uwasa) Mhandisi Joshua Mgeyekwa alikiri kuwepo kwa uharibifu mkubwa katika vyanzo hivyo unaosababishwa na wananchi katika maeneo hayo.

 
Shughuli za uchimbaji wa dhahabu,kilimo na maogesho ya mifugo katika vyanzo hivyo vimekuwa vikichangia kwa kiasi kikubwa kuongeza matope kwenye bwawa la Mabayani linalosambaza maji Mjini hasa kipindi hiki cha mvua za masika.

   
Mamlaka hiyo ilikuwa inazalisha maji kiwango cha ujazo km 29,000 na kupungua hadi kufikia ujazo wa km 20,000 kwa sasa jambo lililopelekea kuanza kutoa huduma hiyo kwa mgao ndani ya Jiji la Tanga.
 

Mkurugenzi huyo alisema tayari mamlaka hiyo imekwisha kuanza kuchukua jitihada za haraka ikiwemo kutumia maji ya kisima cha mwakileo ambacho kina uwezo wa kutoa maji kwa ujazo wa km 30,000 hadi 35,000 ambayo yanaweza kukidhi mahitaji ya zaidi wananchi 47,000 kwa wakati mmoja sambamba na kuzibua mabomba ambayo yamekuwa na tope iliyosababishwa na mvua zinazoendelea sasa.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.