NAIROBI:MKUTANO WA MAKAKATI KAZI WA MAWASILIANO WA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO WAANZA JIJINI NAIROBI
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Duniani Costa Williams |
Baadhi ya wajumbe toka Tanzania |
Mkutano wa Mkakati kazi Wa Idara ya Mawasiliano katika Kanisa la Waadventista Wa Sabato katika kanda ya Africa Mashariki na Kati (ECD) unaohusisha viongozi Wa Idara hiyo pamoja na Vituo vya Habari vya Habari umeanza hii Leo jijini Nairobi nchini Kenya.
Mkutano huo unaowaunganisha Wakurugenzi Wa Idara ya Mawasiliano pamoja na wasimamizi Wa vituo vya habari vya kanisa katika kanda hiyo unaongozwa Na Mkurugenzi Wa Idara hiyo katika ngazi ya Ulimwenguni Costa Williams.
Williams amesisitiza juu ya matumizi ya maneno katika injili kupitia mitandao ya kijamii,Redio,Televishen na katika Mazungumzo na namna ya kukabiliana na Majanga katika kanisa. Lengo kuu la mkutano huo ni kupanga mikakati ya kanisa kupitia Idara ya mawasiliano kwa miaka 5.
Post a Comment