MWANZA:MWENYEKITI WA BODABODA MKOANI MWANZA ATOA TAHADHARI JUU YA VITENDO VYA UKWAPUAJI
Mwenyekiti
wa Chama cha Waendesha Pikipiki Mkoani Mwanza Makoye Kayanda (pichani), amewataharisha
wakazi wa Jiji la Mwanza kuwa makini wawapo barabarani, ili kuepukana na
vitendo vya ukwapuaji wa Mikoba na Mabegi vinavyofanywa na baadhi ya wahalifu
kwa kutumia pikipiki.
Kayanda alitoa tahadhari hiyo jana Mwanza baada ya kupokea
malalamiko ya kukithiri kwa vitendo vya ukwapuaji vinavyofanywa na baadhi ya
watu wanaojifanya waendesha pikipiki, jambo linalochafua taswira ya waendesha
pikipiki Mkoani Mwanza.
Tayari watu kadha wamefikisha malalamiko yao kwa uongozi wa bodaboda Mkoani Mwanza, baada ya kukumbwa na
kadhia ya kukwapuliwa mikoba pamoja na mabegi yao, ambapo mmoja wa wahanga wa
matukio hayo Diana Abdallah ameeleza kukwapuliwa mkoba wake uliokuwa na pesa
pamoja na vito vya thamani wakati akitokwa kwenye shughuli zake.
Post a Comment