SHINYANGA:WAIMBAJI WAWILI WAKONGWE WA SAUTI YA JANGWANI WAFARIKI DUNIA
Wa Kwanza mstari wa nyuma ni Marehemu Mery Petro enzi za uhai wake |
Waimbaji wa Sauti ya Jangwani walipokuwa kwenye makambi ya Manzese 2015 |
Toka juma lililopita yaani ijumaa ya Septemba 25,2015 na usiku wa ijumaa ya Oktoba 2,2015 kwaya ya
Sauti ya Jangwani toka Shinyanga imejikuta ikiwapoteza waimbaji wake wakongwe
ambao wamelala mauti.
Mery Petro (wa kwanza kulia mstari wa nyuma picha ya pili) ambaye alikuwa
anasumbuliwa na Kansa ya Kizazi alizikwa Septemba 25 mwaka huu huko Shinyanga,ijumaa ya
Oktoba 2 usiku wa kuamkia leo Mwimbaji mwingine Suzana Kigocha amefariki dunia
katika Hospitali ya Bugando jijini Mwanza alikokuwa amelazwa.
Mwili wa Marehemu Suzana Kigocha unataraji kufikisha leo
mjini Shinyanga kwa ajili ya taratibu za maziko yatakayofanyika huko
Kolandoto,Shinyanga.
Sendama John toka Shinyanga amezungumza na blog hii kuhusu
tukio hilo mapema leo
Post a Comment