MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:WATANZANIA WATAHADHARISHWA KUHUSU MADHARA YA KEMIKALI

 

Serikali ya Tanzania kupitia wakala wa Maabara ya Mkemia mkuu wa serikali ya nchi hiyo imeeleza kuwa katika kipindi cha mwaka jana jumla ya matukio na ajali za kemikali zipatazo 11 zilitolewa taarifa na zilisababisha vifo zaidi ya watu 14 pamoja na uharibifu mkubwa wa mali ikiwemo kuungua moto magari na tani zaidi ya 250 za kemikali pia kuteketea kwa moto.

Taarifa hiyo inaeleza kuwa kemikali wanazokutana nazo watanzania zinatoka katika vyakula,dawa wanazokunywa,nguo wanazovaa,maji ya kunywa na sehemu mbalimbali za kazi,viwandani na mashambani.

Meneja wa maabara ya Kanda ya Afrika Mashariki  Daniel Ndiyo amefafanua kuwa  serikali iliamua kutunga sheria ya usimamizi wa udhibiti wa kemikali za viwandani na majumbani lengo likiwa ni kuhakikisha kemikali zinatumika vizuri kama anavyoeleza hapa.
 

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.