DAR ES SALAAM: MKE WA RAIS WA TANZANIA MAMA SALMA KIKWETE AWATAKA WANASIASA KUTOENEZA SIASA ZA CHUKI NCHINI HUMO
Mama Salma Kikwete akiwa na Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mch Mark Walwa Malekana |
Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono wananchi waliohudhuria tamasha la kuombea amani Tanzania |
Mama Salma Kikwete akihutubia |
Mama Salma Kikwete akipokea tuzo ya Rais Jakaya Kikwete toka kwa Mch Mark Walwa Malekana iliyotolewa na Kampuni ya Msama Promotion |
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Paul Makonda akihutubia kwenye Tamasha la Kuombea Amani Tanzania lililofanyika Uwanja wa Taifa Oktoba 4,2015 |
Mke wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mama Salma Kikwete amewataka wanasiasa na wafuasi wao kutoeneza siasa za chuki ambazo zinaweza kuwatenga wananchi kwa misingi ya dini,ukabila,ukanda kwa kuwa jambo hilo ni hatari kwa taifa la Tanzania pia kutofanya kampeni katika nyumba za ibada.
Mama Salma Kikwete alitoa agizo hilo wakati akihutubia maelfu ya waumini wa madhehebu ya mbalimbali ya dini nchini Tanzania katika Tamasha la Kuombea Amani kabla ya uchaguzi mkuu wa Oktoba 25 mwaka huu lililofanyika kwenye uwanja wa michezo wa Taifa jijini Dar es salaam Oktoba 4,2015 ambapo pia lililowahusisha viongozi wa madhehebu hayo na waimbaji wa nyimbo za injili toka Tanzania,Kenya,Zambia,Afrika Kusini na Uingereza.
Naye Kiongozi wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji Mark Walwa Malekana akikabidhi tuko ya Rais Jakaya Kikwete kwa Mama Kikwete amesema amani ya Tanzania italetwa kwa maridhiano na kuheshimiana.
Post a Comment