DAR ES SALAAM:TAARIFA YA KONGAMANO LA KIMATAIFA LA UTAFITI WA MAGONJWA YA BINADAMU HII HAPA
Kongamano
la Wanasayansi lililoandaliwa na Taasisi ya
Magojwa ya Binadamu nchini Tanzania linatarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere
jijini Dar es salaam.
Mkurugenzi wa
Taasisi ya Utafiti wa Magojwa ya Binadamu Tanzania Dr Mwele
Malecela (Pichani) amesema lengo la Kongamano hilo ni
kuwakutanisha watafiti,watunga Sera,watoa maamuzi,wananchi na wadau
wengine wa tafiti za afya kutoka ndani na nje ya Tanzania ili kuwakisisha
na kujadili matokeo ya Tafiti mbalimbali za uimarishaji wa afya na hali
bora ya Maisha.
Malecela
amesema kongamano hilo litaambatana na Maadhimisho ya miaka 35 ya taasisi
ya taifa ya utafiti wa magojwa ya binadamu na Kumbukumbu za miaka 120 za
utafiti wa Afya Tanzania na mada zitakazozungumziwa zitalenga Tafiti za
magojwa,mifumo ya huduma za Afya na Visababishi vya Maradhi katika
Jamii.
Post a Comment