NAIROBI:MO DEWJI MFANYABIASHARA TOKA TANZANIA ANYAKUA TUZO YA MWAKA YA MFANYABIASHARA ANAYESAIDIA ZAIDI JAMII
Mkurugenzi
Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker akimkabidhi tuzo ya '2015
Philanthropist of the year-East Africa' Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni
ya MeTL Group, Mohammed Dewji katika sherehe zilizofanyika hoteli
ya DusitD2 jijini Nairobi.(Picha zote na Zainul Mzige wa Modewjiblog).
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akizungumza
kwenye hafla ya tuzo za All Africa Business Leaders Awards 2015 (AABLA).
Kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akipozi katika
picha ya kumbukumbu na Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta
Naicker.
Afisa Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akiwa ameshikilia tuzo yake.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji akibadilishana
mawazo na baadhi ya wafanyabiashara wakubwa jijini Nairobi ambapo pia
walimpongeza.
Afisa
Mtendaji Mkuu wa Makampuni ya MeTL Group, Mohammed Dewji katika picha
ya kumbukumbu na mmoja wa wageni waalikwa kwenye hafla ya tuzo za All
Africa Business Leaders Awards 2015 zilizofanyika kwenye hoteli ya Dusit
D2 jijini Nairobi.
Mohammed Dewji, CEO of MeTL Group....2015 Philanthropist of the Year-East Africa.
Na Mwandishi Wetu
Bilionea anayemiliki kampuni kubwa ya Mohammed Enterprises nchini Tanzania (MeTL),
Mohammed Dewji `Mo’ ameshinda Tuzo ya Mfanyabiashara wa Mwaka anayejitoa
zaidi kuisaidia jamii kutokana na biashara zake, akiwa
mshindi wa Afrika, Kanda ya nchi za Afrika Mashariki katika tuzo
zilizofanyika juzi jijini Nairobi, Kenya.
Katika
tuzo hiyo ya heshima kwa wafanyabiashara Afrika inayoratibiwa na Kituo
cha Biashara cha Televisheni ya CNBC Afrika, Dewji alishindanishwa na
mabilionea raia wa Kenya, Ashok Shah wa kampuni ya Apollo Investment
Limited na Damaris Too-Kimondo anayemilikia kampuni ya Shrand
Promotions.
Katika sherehe hizo zilizofana, Dewji alikabidhiwa tuzo yake na Mkurugenzi Mtendaji wa CNBC Africa, Roberta Naicker.
Ushindi
wake umechangiwa kwa kiasi kikubwa na kitendo cha Dewji ambaye pia ni
mwanasiasa aliyekuwa mbunge wa Singida Mjini kwa miaka kumi, kujihusisha
na misaada yenye lengo la kupambana na umasikini kupitia sekta
mbalimbali kama elimu, maji, watu wenye ulemavu na pia uwezeshaji
kiuchumi, matukio ambayo yamelenga na kubadili hali ya watu maskini
zkatika jamii.
Washindi
hao wa Kanda ya Afrika Mashariki watashindanishwa na washindi wengine
kutoka Kanda ya Kusini mwa Afrika na Afrika Magharibi Novemba 13, mwaka
huu huko Sandton, Johannesburg nchini Afrika Kusini ili kupata mshindi
wa jumla wa bara la Afrika.
Akizungumza
mara baada ya kutunukiwa tuzo yake hiyo yenye heshima kubwa,
aliwashukuru waandaaji, jarida la Forbes na majaji kwa kumuona
anastahili kwa tuzo hiyo ya kipekee.
Alisema,
kwake ni faraja kubwa kupata heshima huyo na amekuwa na ndoto za
kusaidia watu wa Tanzania kukabiliana na changamoto wa kasi ya maendeleo
barani Afrika na kwamba ili kuendana na kasi hiyo, miongoni mwa juhudi
zinazotakiwa ni kuwawezesha kupata elimu bora, hasa wa maeneo ya
vijijini.
Dewji
mwenye umri wa 40 ambaye kwa sasa ndiye bilionea kijana zaidi Afrika
kwa vijana wasiozidi umri huo, akiwa pia miongoni mwa mabilionea 55
wanaoongoza kwa utajiri Afrika, anaongoza kampuni yenye makampuni
yaliyojikita katika sekta za kilimo, fedha, uzalishaji, usambazaji wa
bidhaa na kadhalika, huku akitajwa kuajiri zaidi ya watu 20,000.
Post a Comment