MOROGORO:RAIS KIKWETE AWAPA POLE MAJERUHI YA MSONGAMANO WA WANANCHI BAADA YA MKUTANO WA KAMPENI KATIKA UWANJA WA JAMHURI MJINI MOROGORO
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
Rufaa ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya alipokwenda kuwapa pole
majeruhi walioumia katika msongamano mkubwa uliotokea katika mlango wa
kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni wa CCM katika Uwanja wa Jamhuri
mjini Morogoro Septemba 6, 2015.
Watu wawili walipoteza maisha,
akiwemo mvulana wa miaka 12 aliyejulikana kwa jina la Ramadhani Abdallah
na mwanamama Grace George (42), ambapo jumla ya watu 17 walijeruhiwa na
kukimbizwa hospitalini hapo. Hadi jana jioni majeruhi saba walikuwa
wameruhusiwa
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Kaimu Mganga Mkuu wa
Hospitali ya Mkoa wa Morogoro Dkt. Samson Tarimo alipokwenda kuwapa pole
majeruhi walioumia katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa
kampeni katika Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi Septemba 6, 2015.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Mweka Hazina wa CCM mkoa wa
Morogoro Ndg. Hassan Bantu alipokwenda kuwapa pole majeruhi walioumia
katika mlango wa kutokea nje baada ya mkutano wa kampeni katika Uwanja
wa Jamhuri mjini Morogoro Septemba 6, 2015.
Mmoja
wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa kitandani pake hospitalini
hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye msongamano huo
Rais
Kikwete akimpa pole mmoja wa majeruhi Bw. Kokoliko Ramadhani akiwa
kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye
msongamano huo
Rais
Kikwete na Mama Salma Kikwete wakimpa pole mmoja wa majeruhi Bi Flora
Maduka akiwa kitandani pake hospitalini hapo baad ya kujeruhiwa katika
msongamano huo
Rais
Kikwete akimpa pole mmoja wa majeruhi Bi. Jalia Mohamed akiwa
kitandani pake hospitalini hapo akiuguza bega la kuume aliloumia kwenye
msongamano huo
Rais Kikwete akiendelea kutoa pole kwa majeruhi
Rais Kikwete akimfariji mmoja wa majeruhi
Rais
Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa
wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyeungua
kwa moto
Rais Kikwete alitumia wasaa huo kuwapa pole wagonjwa wengine waliokuwa
wamelazwa wodi moja na majeruhi hao. Hapa anamfariji mtoto aliyevunjika
mguu wakati akicheza kwenye mti
Rais
Kikwete akimpa pole mvulana ambaye aligongwa na gari wakati akielekea
kumsikiliza mgombea Urais kwa tiketi ya CCM Dkt John Pombe Magufuli
katika mkutano wa kampeni Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro juzi
Rais Kikwete alipata fursa ya kutembelea wodi ya watoto na kuwapa pole kwa kuumwa kwao
Rais Kikwete akiongea na wanafunzi waliokuwepo hospitalini hapo kumtembelea mgonjwa
Rais Kikwete akizungumza na wananchi
Rais
Kikwete akitoa mapendekezo ya kupanua hospitali hiyo ambayo ina eneo
kubwa lakini majengo machache ya chini. Alipendekeza uongozi wa
hospitali na mkoa ubuni namna ya kuipanua kwa kujenga majengo ya ghorofa
ili kuwepo na wodi na sehemu nyingi zaidi za huduma.
Mwishoni
Rais Kikwete aliongea na wanahabari wa kutoka vyombo mbalimbali na
kueleza masikitiko yake kwa yaliyotokea jana Uwanja wa Jamhuri baada ya
mkutano wa kampeni kumalizika.
Rais
Jakaya Kikwete akiongea na Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Rufaa ya
Mkoa wa Morogoro Dkt. Ritha Lyamuya baada ya kuwajulia hali majeruhi wa
msongamano baada ya mkutano wa kampeni uwanja wa Jamhuri Morogoro jana. (Picha na Ikulu)
Post a Comment