MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:VIONGOZI WAPYA WA UNIONI YA KUSINI MWA TANZANIA YA KANISA LA WAADVENTISTA WASABATO HAWA HAPA


Mwenyekiti Mpya wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mch Mark Walwa Malekana


Katibu Mkuu Mpya wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mch Rabson Nkoko akiwa na mkewe

Mhazini wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania Jack Manongi (katikati mwenye miwani)

Kanisa la Waadventista Wa Sabato Unioni ya Kusini mwa Tanzania limepata viongozi wapya watakaoiongoza unioni hiyo  katika kipindi cha miaka mitano ijayo.


Viongozi hao watatu waliochaguliwa jana na mkutano mkuu wa kanisa hilo unaojumuisha wajumbe toka nchi 11 uliofanyika yalipo makao makuu ya  Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati (ECD) Ongata Rongai ni Mchungaji Mark Walwa Malekana kuwa Mwenyekiti wa Union ya Kusini Mwa Tanzania.


Akitoa taarifa kwa njia ya Simu Mkurugenzi wa mawasiliano wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji Stephen Letta amesema viongozi wengine waliochaguliwa ni Mchungaji Rabson Nkoko kuwa Katibu Mkuu na Jack Manongi ambaye anaendelea kuwa  uhazini wa Unioni hiyo.

Mchungaji Magulilo Mwakalonge ambaye alikuwa mwenyekiti wa Unioni ya Kusini mwa Tanzania amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Vijana wa Divisheni ya Afrika Mashariki na Kati (ECD).


 Unioni ya Kusini mwa Tanzania katika kanisa la Waadventista Wa Sabato inajumuisha mikoa ya Dar es salaam,Pwani,Morogoro,Lindi,Mtwara,Katavi,Mbeya,Dodoma ,Rukwa,Iringa,Njombe,Unguja na Pemba 


Mkutano huo unaotarajiwa kumalizika hii leo ni kwa ajili ya kupanga mikakati na mipango ya kazi katika kipindi cha miaka mitano ikiwemo kuchagua wasaidizi wa maofisa wa ngazi za juu,wakurugenzi wa idara 10 za  Divisheni hiyo na maofisa watatu wa kila unioni nane zilizopo kwenye divisheni ya Afrika Mashariki na Kati.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.