SINGIDA:MO DEWJI FOUNDATION YAKABIDHI MATUNDU NANE YA CHOO BORA KWENYE SHULE YA MSINGI KIBAONI
Mwalimu
 mkuu wa shule ya msingi Kibaoni mjini Singida, Sundi Samike, 
akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane 
chenye thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni zilizotolewa na MO Dewji 
Foundation (shilingi 14 milioni) na Doris Mollel Foundation shilingi 2.3
 milioni).
Mwakilishi
 wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, akizungumza 
kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane shule ya msingi 
Kibaoni mjini Singida, chenye thamani ya zaidi ya shilingi  milioni 16. 
Duda amewataka wakazi wa manispaa ya Singida, kujenga utamaduni wa 
kuchangia kwa hali na mali, uboreshaji wa mazingira ya shule, ili 
kuvutia wanafunzi kupenda shule.
Mkurugenzi
 wa Doris Mollel Foundation ya jijini Dar-es-sa-laam, Doris Mollel, 
akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora chenye matundu nane ya 
shule ya msingi Kibaoni mjini Singida chenye thamani ya zaidi ya 
shilingi 16 milioni, kati ya fedha hizo, Mo Dewji Foundation imetoa 
shilingi 14 milioni na Doris Foundation shilingi 2.3 milioni.
Mwakilishi
 wa Mo Dewji Foundation mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa tatu kulia) 
akiteta jambo na Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundation, Doris Mollel (wa
 pili kulia) wakielekea kuzindua choo bora kipya cha shule ya msingi 
Kibaoni.
Mwakilishi
 wa MO Dewji mkoani Singida, Duda Mughenyi, (wa pili kushoto) na 
Mkurugenzi wa Doris Mollel Foundatin, Doris Mollel (wa tatu kushoto) kwa
 pamoja  wakizindua choo bora kipya cha shule ya msingi Kibaoni chenye 
thamani ya zaidi ya shilingi 16 milioni. MO Dweji Foundation imechangia 
shilingi 14 milioni na Doris Mollel, shilingi 2.3 milioni.
Jengo
 la choo bora chenye matundu nane kilichojengwa kwa thamani ya zaidi ya 
shilingi 16 milioni kwa ushirikiano wa MO Dewji Foundation na Doris 
Mollel Foundation kitakachotumiwa na wanafunzi 842 wa shule ya msingi 
Kibaoni mjini Singida. (Picha na Nathaniel Limu).
Wazazi,Walezi na Wakazi wa  halmashauri ya manispaa ya Singida, wamehimizwa kujenga 
utamaduni wa kuchangia kwa hali na mali uboreshaji wa mazingira ya 
shule, kama njia moja wapo ya kuwavutia wanafunzi kuhudhuria shule.
Wito
 huo umetolewa na Mwakilishi wa MO Dewji Foundation mkoa wa Singida, 
Duda Mughenyi, wakati akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi choo bora 
chenye matundu  nane chenye  thamani ya zaidi ya shilingi milioni 16 kwa
 shule ya msingi Kibaoni mjini hapa,  yenye jumla ya wanafunzi 842, kati
 yao wavulana ni 377 na wasichana ni 465.
Alisema
 uzoefu unaonyesha kwamba mazingira ya shule yakiwa safi, vifaa vya 
kufundishia na kujifunzia viwepo vya kutosha , maji safi na salama 
yawepo na vyoo bora vinavyokidhi mahitaji, hatua hiyo huwajengea 
mazingira mazuri wanafunzi , kujiendeleza kielimu.
Akifafanua,
 alisema shule ya msingi ya Kibaoni ilikaribia kufungwa kutokana na 
kukosa vyoo kwa ajili ya wanafunzi na wanafunzi,lakini Dewji Foundation 
na Doris Mollel Foundation, ilinusuru shule hiyo isifungwe baada ya MO 
Dewji Foundation kutoa shilingi 14 milioni na Doris Mollel kutoa 
shilingi 2,300,000.
Duda alitumia nafasi hiyo kuwataka wanafunzi wakitunze na kudumisha usafi wa choo hicho ili kiweze kutumika kwa muda mrefu.
Kwa
 upande wake Doris Mollel (Miss Singida 2014), alisema Foundation yake 
itaendelea kufadhili sekta ya elimu mkoani Singida kama njia ya 
kuwashukuru wakazi  mkoani hapa kwa kumsapoti na kufanikisha kushinda 
nafasi ya Miss Singida mwaka jana.
Awali
 Mwalimu mkuu wa shule ya msingi Kindai tarafa ya Mungumaji 
iliyoanzishwa mwaka 1975,Sundi Samike,alishukuru uongozi wa Mo Dweji 
Foundation na Doris Mollel Foundation, kwa kuifadhili shule hiyo ujenzi 
wa choo na kuinusuru kufungiwa.
“Nitumie
 nafasi hii pia kulipongeza shirika la WaterAid Tanzania kwa uamuzi wake
 wa kufadhili ujenzi wa vyoo bora ambao ujenzi wake tayari 
umeishaanza.Aidha,nitoe wito kwa wazazi,wasaidie kwa hali na mali 
kuharakisha ujenzi huu”,alisema.


Post a Comment