MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:TBS KUFANYA MSAKO MKALI NCHI NZIMA KUWABAINI WAUZAJI WA UMEME NURU 'SOLAR POWER PANELS' ZILIZO CHINI YA KIWANGO


 Katibu  Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew Matimbwi (katikati), akiwaonesha wanahabari Dar es Salaam leo asubuhi Umeme Nuru (Solar Power panels) ambazo hazina ubora zilizokamatwa zikiwa katika soko la Tanzania baada ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kwa kushirikiana na Taasisi hiyo, kufanya uchunguzi na kubaini kuwepo katika soko solar hizo. Kulia ni Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe  na Ofisa Uhusiano, Roida Andusamile.


 Katibu  Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew, akiwaonesha wanahabari Solar Power panels zinazotakiwa kuwa kwenye soko ambazo ni bora.
  Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari Makao Makuu ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS), Ubungo Dar es Salaam leo asubuhi kuhusu shirika hilo kuanza msako mkali wa kuwabaini wafanyabiashara wanaouza Umeme Nuru (Solar Power Panels), zilizochini ya kiwango. Kulia ni  Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe na Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Ashura Katunzi.
 Ofisa Udhibiti Ubora wa TBS, Ashura Katunzi akisisitiza jambo wakati akizungumza na wanahabari. Kutoka kushoto ni Ofisa Masoko Mwandamizi wa TBS, Gladness Kaseka,Katibu  Mtendaji wa Taasisi ya Nishati Jadidifu (TAREA), Mhandisi Mathew Matimbwi, Ofisa Uhusiano wa TBS, Roida Andusamile.
 Ofisa Viwango wa TBS, Henry Massawe akizungumza katika mkutano huo.
Wanahabari na wadau wengine wakiwa kwenye mkutano huo.

Shirika  la viwango Tanzania TBS kwakushirikiana na Taasis ya Nishati Jadidifu (TAREA) iliamua kufanya ukaguzi wa kushtukiza kufuatia malalamiko mengi kuhusiana na ubora waVipande vyaumemenuru katika soko la Tanzania ilikutatuatatizo. Mnamo  juni  23,2015, TBS ilifanya ukaguzi wa Umeme Nuru (Solar Power Panels) katika maeneo yafuatayo;
Keko- Mwanga, MtaawaMsimbazi, Mtaawa Congo. 

 TBS ilibaini baadhi
ya wasambazaji  walikuwa na bidhaa za umeme nuru zilizo chini ya kiwango nyingi zikitokea nchini China.

Jumla ya vipande vya umemenuru 1321 kutokaduka na ghala la Regal Solar Ltd vilizuiwa kuuzwa; na 164 kutokaduka la Nishati Electronics Ltd pia vilizuiwa kuuzwa baada ya ubora wake kutiliwa shaka mpaka matokeo ya maabara yatakapotoka. 
Na vile vile wakaguzi walichukua sampuli kutokaduka la Keoali Power & EquipmentsCo.Ltd.

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.