DAR ES SALAAM:WASI WASI WA MVUA ZA EL-NINO NCHINI MWEZI SEPTEMBA MPAKA DESEMBA MWAKA HUU-TMA
Nchi za Afrika
Mashariki na kati ikiwamo Tanzania zipo katika wasiwasi wa kukumbwa na mvua za
El-nino kutokana na kuongezeka kwa joto katika Bahari ya Pacific.
Akizungumza
kwenye mkutano wa 41 wa masuala ya hali ya hewa na utabiri unaofanyika jijini
Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dk. Agness
Kijazi (pichani) amesema kitaalam kuna uwezekano
wa kutokea kwa mvua kubwa katika nchi za Afrika Mashariki katika kipindi cha
Septemba mpaka Desemba, mwaka huu.
Mkutano huo
unawahusisha wataalam mbalimbali kutoka katika nchi 11 na unaangalia mifumo ya
hali ya hewa kwa Afrika Mashariki na tayari wameona viashiria vya kutokea kwa
mvua hizo.
Amesema baada ya
kuangalia mifumo ya hali ya hewa katika eneo la Afrika Mashariki, wataalamu
watarudi katika nchi zao na kuangalia mifumo ya hali ya hewa katika maeneo yao
na kutoa utabiri kwa wananchi husika kwa kipindi cha mwez Septemba mpaka
Desemba.
Kijazi ametoa
wito kwa wananchi na wadau wa hali ya hewa kufuatilia utabiri utakaotolewa
Septemba Mosi, mwaka huu ili kujua hali itakavyokuwa.
Post a Comment