MTANGAZAJI

SONGEA:MGOMBEA URAIS DR MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA KAMPENI RUVUMA KUANZIA




 

Mgombea Urais kupitia chama cha Mapinduzi (CCM) Dr. John Magufuli anatarajiwa kupokelewa na mamia ya wananchi wakiwemo wanachama wa chama cha mapinduzi katika kijiji cha Igawisenga wilayani Songea mkoa wa Ruvuma akitokea mkoa wa Njombe  tayari kuanza kampeni mkoani humo.

Akizungumza na waandishi wa habari jana kwenye ofisi za chama cha mapinduuzi mkoani Ruvuma Mwenyekiti wa  kamati ya maandilizi ya kampeni mkoani Ruvuma ya mgombea uraisi wa jamhuri ya mungano wa Tanzania Dr. Magufuli, Wabunge na Madiwani Ramadhani Kayombo alisema kuwa Dr. Magufuli na msafara wake unatarajiwa kupokelewa Agost 30 mwaka huu majira ya asubuhi huko katika kijiji cha Igawisenga.
Kayombo alieleza kuwa chama cha mapinduzi kimejipanga kikamilifu kwa kuhakikisha kuwa Dr. Magufuli, Wabunge na Madiwani wanafanyiwa kampeni za kistaarabu katika kipindi chote cha kampeni ambapo mgombea uraisi Dr. Magufuli anatalajia kufanya ziara za kampeni katika wilaya za Nyasa, Mbinga, Songea, Namtumbo na Tunduru ambako atamaliza ziara Septemba 02 mwaka huu na kuendelea na ziara mkoani Mtwara.
Alisema kwa kuwa wananchi wengi wana imani na chama cha mapinduzi ambao wanahitaji kumuona na kumsikiliza  hivyo amewataka wajitokeze kwa wingi kwenye mikutano ya hadhara ya kampeni itakayofanyika wakati Dr. Magufuli akiwa mkoani Ruvuma na amewaomba kuwa na mshikamano wa pamoja katika kuhakikisha kuwa chama cha mapinduzi kwenye uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika oktoba 25 mwaka huu kinapata ushindi wa kishindo kwa mgombea uraisi, wabunge na madiwani na si vinginevyo.
 Na Jamvi la Habari- Songea 


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.