MTANGAZAJI

KIONGOZI WA UPINZANI NCHINI GHANA ASEMA ANALIPENDA KANISA LA WAADVENTISTA WA SABATO

Nana Addo Akufo Addo akipokea zawadi ya kitabu



Kiongozi wa upinzani nchini Ghana  Nana Addo-Dankwa Akufo-Addo,ambaye ni mwanglikana ameeleza hisia zake za kulipenda kanisa la waadventista Wa Sabato ambapo aliamua  kusali katika kanisa la waadventista la Mashariki mwa London sabato iliyopita baada ya kutembelea nchini Uingereza.

Akufo-Addo mwanasheria maarufu na aliyewahi kuwa waziri wa mambo ya nchi za nje wa Ghana alifika katika kanisa hilo julai 25 mwaka huu akiwa ameambatana na wafuasi wake toka nchi za Uingereza na Ireland.

Alishiriki katika ibada ya sabato hiyo kwa nyimbo,maombi na mahubiri yaliyoendeshwa na Mchungaji Msaidizi wa Kanisa hilo Joojo Bonnie aliyehubiri kuhusu kisa cha Gidioni ndani ya Biblia katika kitabu cha waamuzi sura ya sita hadi ya nane.

Mchungaji kiongozi  Fergus Owusu Boateng,alitoa ombi maalum kwa kiongozi huyo na baada ya hapo alipewa zawadi ya kitabu kilichoandikwa na  Ellen G. White.

Kanisa la Waadventista Wa Sabato huwa halijihusishi na mambo ya kisiasa lakini huwa liko tayali kuomba hekima ya MUNGU kwa ajili ya wale walioko madarakani.
Akufo-Addo mwenye umri wa miaka 71 ambaye anapanga kugombea urais mwakani aliomba viongozi wa kanisa kuombea amani nchini Ghana.


No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.