DAR ES SALAAM:KAMATI YA TUZO YA JAMII YATEMBELEA NA KUKAGUA UKUMBI WA JULIUS NYERERE INTERNATIONAL CENTRE (JNICC)
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Jamii D.J Malegesi akizungumza na Mratibu wa Tuzo ya Jamii Amani Mwaipaja ndani ya ofisini za JNICC |
Ndani ya Ukumbi |
Mwenyekiti wa Kamati ya Tuzo ya Jamii D.J Malegesi akiwa na Mratibu wa Tuzo ya Jamii Amani Mwaipaja wakiwa nje ya ukumbi wa JNICC |
Tuzo ya Jamii ni Tuzo inayotolewa kwa Taasisi na watu binafsi kutokana na jitihada na mchango wao katika kusaidia na kutetea maslahi ya Jamii.
Tuzo ya Jamii huandaliwa na kutolewa na Tanzania Awards International LTD na hutolewa Aprili 13 ya kila mwaka kwa kuwa siku hiyo ndiyo aliyozaliwa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere Rais wa Kwanza wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Kwa mwaka huu Tuzo ya Jamii itatolewa katika vipengele vitatu ambavyo ni;
1.Tuzo ya Jamii-Tuzo ya Heshima watakayopewa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Nelson Mandela Rais wa Kwanza Mzalendo wa Afrika ya Kusini.
2.Tuzo ya Haki za Binadamu itakayotolewa kwa mshindi atakayetangazwa siku ya Tuzo
3.Tuzo ya Jamii ya Mwanasiasa mwenye mafanikio katika siasa za Tanzania.Kipengele hiki kitakuwa na washindi wawili Kijana mmoja na Mtu mzima mmoja ambao watapatikana baada ya kupendekezwa kupitia mtandao wa Push Mobile ambapo wananchi watashiriki kupendekeza jina la mwanasiasa kwa kuandika neno TUZO katika sehemu ya ujumbe mfupi
wa maneno,wataacha nafasi kisha watapendekeza jina na ujumbe huo watautuma kwenda namba 15522.
Hafla ya utoaji wa Tuzo ya Jamii kwa mwaka huu itafanyika katika ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere International Conversion Centre (JNICC) ulioko jijini Dar es salaam.
Post a Comment