MBEYA:MCHUNGAJI RABSON NKOKO ACHAGULIWA MWENYEKITI MPYA WA SHC
Mkurugenzi
wa mawasiliano wa kanisa la Waadventista Wa Sabato Unioni ya kusini mwa
Tanzania Mchugaji Rabson Nkoko (Pichani) amechaguliwa hii leo kuwa mwenyekiti mpya wa Konferensi ya Nyanda za juu Kusini mwa
Tanzania ya Kanisa hilo (SHC)
Uchaguzi
huo unafuatia mabadiliko yaliyofanyika hivi karibuni ya kuundwa kwa konferensi
mbili mpya baada ya kuvunjwa kwa iliyokuwa
konferensi ya mashariki mwa Tanzania ambapo aliyekuwa mwenyekiti wa
konferensi hiyo Mchungaji Joseph Mngwabi alichaguliwa kuwa mwenyekiti mpya wa
konferesi ya Mashariki na kati mwa Tanzania.
Mkurugenzi
wa mawasiliano konferensi ya nyanda za juu kusini Mchungaji Haruni Kikiwa
ameiambia Morning Star Radio kuwa zoezi la uchaguzi huo lilianza kwa kuundwa kwa
kamati ndogo ya uchaguzi ambayo ilikamilisha zoezi hilo majira ya saa sita
mchana na kumtangaza mwenyekiti huyo.
Hii
itakuwa ni mara ya kwanza kwa Mchungaji Nkoko kushika wadhifa huo,ambapo amewahi
kuwa Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Unioni ya Tanzania na iliyokuwa Taasisi ya
Vyombo vya Habari vya Kanisa la Waadventista Wa Sabato (TAMC) na Mchungaji wa
Mtaa wa Kinondoni.
Akizungumza
na Morning Star Radio mara baada ya uteuzi huo Mchungaji Nkoko amesema amepokea
wadhifa huo kwa unyenyekevu na ameahidi kushirikiana na viongozi wengine katika
kuwahimiza washiriki wa konferensi hiyo kumtafuta Mungu ambaye ndiye chanzo cha
mafanikio.
Konferensi
ya Nyanda za Juu Kusini mwa Tanzania ya Kanisa la Waadventista Wa Sabato (SHC)
inawashiriki 46,000 na inajumuisha mikoa sita ya Tanzania bara.
Post a Comment