DAR ES SALAAM:JAMII YATAKIWA KUTOWADHALILISHA WENYE ULEMAVU
Miriam Chirwa akiimba |
Mtaalamu wa malezi ya watoto wa shule ya Uhuru
mchanganyiko Mwalimu Betha Kayola ameitaka jamii kuacha kutumia majina ya
kuwadhalilisha watu wenye ulemavu.
Akizungumza mara baada ya ibada katika kanisa
la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai jana ambako kulikuwa na sabato
maalum ya idara ya watoto, ambayo iliwaalika watoto wenye ulemavu kutoka shule
ya uhuru mchanganyiko ya jijini Dar es salaam amesema kuwa, utumiaji wa majina
yasiyofaa kwa watu wenye ulemavu ni kuwadhalilisha.
Mbali na maneno hayo ya udhalilishaji mtaalamu
huyo amesema kuwa vitendo vya
udhalilishaji vimekuwa vikiendelea ndani ya jamii ambapo baadhi ya wazazi na
walezi wamekuwa wakiwaficha watoto wenye ulemavu na hata kuwafanyia vitendo vya
ukatili hivyo akaomba makanisa ya Waadventista Wa Sabato kuwa karibu na kituo
hicho katika kuwasaidia watoto wa shule ya uhuru Mchanganyiko.
Jumla ya watoto 55 na walezi watatu toka Shule ya Uhuru Mchanganyiko walihudhuria
katika sabato hiyo ya wageni ambayo iliongozwa
na watoto wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Magomeni Mwembechai ambapo Mtoto
mwenye ulemavu Miriam Chirwa aliimba.
Post a Comment