MTANGAZAJI

DAR ES SALAAM:KIONGOZI WA WAADVENTISTA WA SABATO AWATAKA WATANZANIA KUENDELEZA MISINGI YA AMANI NA UPENDO

 

Mwenyekiti wa Kanisa la Waadventista Wa Sabato Unioni ya Kusini mwa Tanzania Mchungaji  Magulilo Mwakalonge amewataka watanzania kuendeleza misingi ya amani na upendo uliyojengwa na waasisi wa taifa hilo bila kujali mila na dini zao.
 
Mwakalonge ametoa agizo hilo mwisho wa juma jijini Dar es salaam alipokuwa akihutubia watu wa dini na madhehebu mbalimbali kwenye sabato ya ujirani mwema iliyofanyika kwenye Kanisa la Waadventista Wa Sabato Tegeta.

 
Amesema watanzania ni watu wanaopenda amani,upendo na kuishi pamoja na imekuwa desturi yao kwa miaka mingi bila kujali tofauti za kidini na mila zao kwa miaka mingi.

 
Kiongozi huyo amesema kuwa watanzania wote ni watoto wa baba mmoja wa mbinguni na wameishi hivyo miaka mingi hivyo analaani vitendo vya kumwagiana tindikali,kurushiana mabomu eti kwa sababu ya tofauti za kidini kwa kuwa havina misingi waliyojengewa watanzania.

 
Amesema zipo kanuni katika maisha ambazo ukitafuta mema kwa watu utayapata hivyo kuna mambo mengi ambayo madhehebu ya dini yanafanana ambayo ndiyo yanapaswa kuhimizwa hivyo kila mtu anapaswa kujifunza kutoka kwa mwenzake kwa yale yaliyo mazu

No comments

Mtazamo News . Powered by Blogger.